Papa Leo XIV atoa wito Ijumaa Agosti 22 iwe siku ya kufunga na kusali ili kuomba amani na haki!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa wito kwa ajili ya kuombea amani, wakati wa salamu, mara baada ya Katekesi yake tarehe 20 Agosti 2025, katika Ukumbi wa Paulo VI. Papa alisema: “Ujumaa ijayo tarehe 22 Agosti tutaadhimisha Kumbu kumbu ya Mwenyejheri Bikira Maria Regina. Maria ni Mama wa Waamini, hapa duniani na anaombwa kama Malkia wa amani. Wakati dunia yetu inaendelea kujeruhiwa na vita nchi Takatifu, Ukraine na katika maeneo mengine mengi ya dunia, ninawaalika waamini wote kutumia siku ya tarehe 22 Agosti katika kufunga na kusali, ili kumwomba Bwana atujalie amani na haki na kukausha machozi ya wale wanaoteseka kwa sababu ya migogoro ya silaha inayoendelea. Bikira Maria, Malkia wa Amani, awaombee watu wapate njia ya amani.”
Papa Laeo XIV vile vile alisalimia wanahija kutoka mataifa mbali mbali kwa lugha mbali mbali na katika lugha ya kiingeraza aliwasalimi kwa namna ya pekee kundi kutoka Uingereza, Finland, Malta, Senegal, Australia, Japan, Korea kusini, Vietnam na Marekani. Papa alisema kuwa “anasali kwamba Jubilei ya Matumaini iweze kuwa wakati wa uponeshaji na wa upyaishwaji kiroho kwa wanawake na wanaume mahali popote.” Na juu yao na familia zao, aliwapatia baraka ya Mungu ya upendo na amani na Mungu awabariki.
Papa Leo XIV pia aliwasalimu kwa wanahija kutoka Italia na sehemu nyingine kwa namna ya pekee watawa waliokuwapo na ambao aliwatia “moyo kushuhudia kwa ari ya kitume kwa karama zao kwa ajili ya manufaa ya Kanisa.” Kisha aliwasalimia vikundi vya parokia, akivihimiza “kila mmoja kuitikia kwa ukarimu mwaliko wa Bwana wa kuwa watangazaji wa furaha wa Injili ya wokovu.” Kwa kuongeza “ Mawazo yangu hatimaye yaliwaelekea vijana, wagonjwa, wanandoa wapya.”
Katika Muktadha wa kumbukizi ya watakatifu wa Kanisa, Papa alisema: “Leo tunaadhimisha siku kuu ya Mtakatifu Bernard wa Clairvaux, Mwalimu wa Kanisa na mwimbaji bora wa nyimbo za Mama Yetu. Yeye ni mtu ambaye aliongoza amani karibu naye, akionesha jinsi ya kuishi Injili. Mfano wake na uwaongoze katika safari yao ya kila siku. Na hatimaye alitoa baraka yake.”
Akiwasalimu mahujaji wa Kipoland waliopo Roma na wale kutoka mahali Patakatifu pa Mama Yetu wa Jasna Góra, huko Poland, ambapo sanamu ya Mama Yetu wa CzÄ™stochowa imehifadhiwa, aliwataka: "kumjumuisha katika nia zao za sala kwa zawadi ya amani ili kunyang'anywa silaha na kupokonywa silaha kwa ulimwengu wote, hasa kwa Ukraine na Mashariki ya Kati."
Hatimaye Baba Mtakatifu mara baada ya kutoka katika ukumbi wa Paulo VI alikwenda nje ya ukumbi huo ambapo aliwakuta waamini katika uwanja akawasalimia na kuwabariki.Mara baada ya kuwabariki aliingia kwenye gari lililompeleka katika Basilika na kuingia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ndani yake, waamini na mahujaji walimsubiri ambao walifuatilia katekesi kupitia skrini zilizowekwa. Papa Leo XIV nao aliwasalimu kwa lugha mbali mbali na kuwabariki.