Papa Leo XIV kwa waendesha Baiskeli:mnakaribishwa daima na Kanisa linalowakilisha upendo wa Mungu kwa watu wote!
Na Angella Rwezaula â Vatican.
Kama ilivyokuwa imepangwa kuhusiana na (Giro dâItalia)mzunguko wa waendesha Basikeli nchini Italia, mpango uliokuwa umekubaliwa hapo awali na Hayati Papa Francisko, Dominika tarehe 1 Juni 2025, saa alasiri, Papa Leo XIV aliwakaribisha ndani ya mji wa Vatican kikundi hicho, kabla ya kuzungukia maeneo ya bustani mjini Vatican. Kwa njia hiyo alitoa maneno mafupi kwao ambapo mwishoni aliwabariki kwa lugha ya kiingereza.
Baba Mtakatifu Leo XIV alisema: Habari za asubuhi kwenu nyote! Karibu Vatican! Ni furaha kuwasalimu kwenye hatua hii ya mwisho ya âGiro d'Italia,â yaani âmzunguko wa Italia.â Ninatumaini kuwa ni siku nzuri sana kwenu nyote. Mjue kwamba nyinyi ni mifano ya kuigwa kwa vijana duniani kote. âGiro d'Italiaâ inapendwa kweli na sio Italia tu. Kuendesha baiskeli ni muhimu sana, kama ilivyo michezo kwa ujumla. Niwakushukuru kwa kila kitu mnachofanya, na ninyi ni mifano ya kuigwa kweli! Na ninatumaini kwamba, kwa kuwa mmejifunza kutunza mwili wenu, roho yenu itabarikiwa kila wakati na kwamba kila wakati mtakuwa makini kwa wanadamu wote: mwili, akili, moyo na roho. Mungu awabariki!â
Mnakaribishwa hapa Vatican
Baba Mtakatifu Leo hakuishia hapo bali hata kwa lugha ya Kiingezea aliwambia kwamba: âMungu awabariki ninyi nyote katika sehemu hii ya mwisho ya âGiro dâItalia.â Hongereni nyote na mjue kwamba mnakaribishwa daima hapa Vatican, mnakaribishwa daima na Kanisa linalowakilisha upendo wa Mungu kwa watu wote. Na baraka ya Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu iwafikie ninyi nyote na kukaa nanyi milele. âWaliitika âAminaâ kwa Baraka hiyo na kuwapongeza wote: âHongereni.â
Waendesha Baiskeli ya Mzunguko wa Italia, baada ya baraka walipata fursa ya kuzungukia Bustani nzuri, kufika hadi, Groto ya Maria wa Lourdes na Monasteri ya Mater Ecclesiae na kurudi nyuma kuendelea na njia yao ya mzunguko uliopangwa.