Papa atawasalimia waendesha baiskeli watakapopitia ndani ya mji wa Vatican
Vatican News
Papa Leo XIV atawasalimia waendesha baiskeli wa “Giro d'Italia,” yaani 'Mzunguko wa Italia' watakapokuwa wanapitia mji wa Vatican Dominika tarehe 1 Juni 2025, saa 9 .30 alasiri. Pia itakuwa ni kufanya kumbukumbu ya Baba Mtakatifu Francisko aliyekubali pendekezo lililowasilishwa na Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na kutekelezwa pamoja na Gavana wa mji wa vatican na Timu ya Kikosi cha Mchezno Vatican. Mpango wa Giro d'Italia kupita Vatican ni "hatua ya kwanza" inayotarajiwa katika Jubilei ya Michezo iliyopangwa kufanyika mnamo Jumamosi tarehe 14 na Dominika 15, iliyozaliwa kunako tarehe 28 Oktoba 2021, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari za Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, wakati wa sherehe ya utoaji wa cheti rasmi cha Riadha ya Vatican na Umoja wa Vyma vya Baiskeli. Na iliwasilishwa mnamo Aprili 29, huko (Campidoglio,)Manispaa ya Roma na Askofu Paul Tighe, katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.
Kuingia kwa waendesha baiskeli mjini Vatican
Kuanza kwa hatua ya mwisho ya toleo la 108 la Giro d'Italia itaanzia katika eneo la Caracalla. Katika hali isiyo ya ushindani, waendesha baiskeli wataingia katika Jiji la Vatican kupitia njia ya Paolo VI Mlango wa Petriano. Njia ndani ya kuta za Vatican yenye urefu wa kilomita 3 hivi: kila mita inasimulia historia na kupendekeza hali ya kiroho, katika mchanganyiko wa sanaa na asili na wanyama mbalimbali na wasiotarajiwa. Waendesha baiskeli hao watakanyaga karibu na basilika na sakristia ya Mtakatifu Petro na kisha kupanda kuelekea Bustani ya Vatican, wakipita mbele ya Kanisa la Mtakatifu Stefano wa Abissini, kituo cha treni, katika eneo la Jumba la Utawala.
Njia ya kuingia na kutokea Mlango wa Perugino
Watapanda zaidi kuelekea monasteri ya Mater Ecclesiae, Grotto ya Mama Maria wa Lourdes, Mnara wa Mtakatifu Yohane hadi Uwanja wa ndege( heliport.) Halafu, kando ya kuta, kwenye njia inayoitwa "njia ya Maria": "safari ya kweli ya ulimwengu" iliyowezeshwa na uwepo wa picha nyingi za Mama wa Mungu zinazoheshimiwa kama watakatifu wa walinzi katika nchi tofauti."Njia ya Marian" inafunguliwa na kazi ya kisanii ya Mama wa shauri jema, pendwa kwa kiroho Wanashirika wa Mtakatifu Agostino. Njia inaendelea kuelekea Bustani ya Uwanja na Makumbusho ya Vatican. Kukiwa na njia iliyojitolea mahususi kwa michezo, hata jina maarufu linakumbuka mbio zilizopendwa na Papa Pio X mwanzoni mwa karne ya ishirini. Waendesha baiskeli kisha watakanyaga kando ya njia ya Fondamenta - katika kivuli cha Kikanisa cha Sistine na karibu na sehemu ya juu ya basilika - kufikia Uwanja wa Mtakatifu Marta na kutoka Jiji la Vatican kupitia Lango la Njia ya Perugino. Mbio za baiskeli zitaanza rasmi katika ardhi ya Italia.