Ujumbe kutoka makanisa duniani wanasali kwa ajili ya Afya Papa Francisko
Vatican News
Katika siku za hivi karibuni, jumbe nyingi za ukaribu na maombi kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu Francisko aliyelazwa katika hospitali ya Agostino Gemelli, jiji Roma tangu tarehe 14 Februari 2025 kutokana na nimonia ya pande mbili, zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku.
Taarifa ya Afya ya Papa
Katika taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imetoa sasisho Alhamis, asubuhi tarehe 20 Februari 2025 kuhusu hali halisi ya Baba Mtakatifu Francisko kuwa: âUsiku ulipita kwa amani, Papa aliamka na kufungua kinywa akiwa ameketi katika sofa.â Katika taarifa ya matibabu iliyotolewa jana jioni tarehe 19 Februari 2025 na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican iliakisi hali "zisizobadilika" na "kuboresha kidogo, hasa uvimbe " unaoneshwa na vipimo vya damu vilivyotathminiwa na wafanyakazi wa matibabu.
Kwa njia hiyo Miongoni mwa Jumbe nyingi hizo kuna barua inayozungumza juu ya: "Ndugu mpendwa Fransisko ninakutakia ahueni ya haraka na kamili, ili kupona haraka, kwa msaada wa Mungu, kwa kazi zako takatifu na muhimu." Barua hiyo imetiwa saini kwa salamu ya kidugu na Patriaki wa Kiekumeni, Bartholomew I, kama ilivyoripotiwa katika barua iliyochapishwa kwenye tovuti ya Upatriaki.
Patriaki wa Yerusalemu
Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, alitoa wito kwa waamini kukusanyika kama familia moja katika imani, iliyounganishwa katika wito wa dhati kwa ajili ya kuombea afya na ustawi wa Papa Fransisko: âKama familia ya kiroho, tumeitwa kuwa pamoja, tukiwa na umoja katika sala na na maombi.â Hayo yamo katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Upatriaki. âTunasali kwa dhati wakati wa Misa, katika nyumba zetu na katika ukimya wa mioyo yetu tukimsihi Bwana amtegemeze Baba Mtakatifu Francisko kwa afya na nguvu mpya, ili aweze kuendeleza utume wake mtakatifu wa kuliongoza Kanisa kwa hekima, unyenyekevu na upendo."
Shirikisho la Maaskofu wa Afrika Mashariki na Madagascar(SECAM)
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar(SECAM limehakikisha "kufuatilia habari za afya ya Papa kwa umakini na kuwa na sala ya dhati kpamoja na mshikamano na ukaribu wa kiroho wa waamini wote."
Ujumbe kutoka Jimbo Kuu la Buones Aires
Mwaliko wa kusali pia umetoka katika ardhi ya asili ya Papa Francisko, kwa Askofu Mkuu Jorge Ignacio García Cuerva wa Jimbo Kuu la Buenos Aires. Katika barua yake aliandika kuwa "Kwa njia hii, tunaonesha upendo wetu kwa Papa Francisko na kumwomba Mungu ampe nguvu kwa ajili ya afya yake na kumuunga mkono katika zoezi ambalo amemkabidhi."
Maombi kutoka Baraza la Maaskofu Canada (CCCB),
Sala zinakuja kutoka Canada kwa ajili ya kupona kabisa kwa Baba Mtakatifu anapoendelea kuliongoza Kanisa kwa ujasiri na ukarimu wa roho. Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Canada (CCCB), William McGrattan, Askofu wa Calgary, kwa niaba ya maasofu wote aliwaaalika kila mmoja, mtu binafsi, familia, haraka na parokia kusali. âBwana, kwa maombezi ya Mama Yetu, ampe nguvu mpya, afya na nguvu katika wito wake wa kulitumikia Kanisa kama Mrithi wa Petro na Mchungaji wa Kristo duniani.â
Kanisa la Lebanon
Nchini Lebanon, Kardinali Béchara Boutros Pierre Raï, Patriaki wa Antiokia ya Wamaroni, alisema kuwa amesali kwa ajili ya Papa Francisko hadharani na faragha: "Bwana na amsaidie, na amponya."
Baraza la Maaskofu nchini Brazil(CNBB)
Urais wa Baraza la Maaskofu wa Brazil(CNBB) umependekeza wakati wa maombi katika siku zijazo kwa ajili ya "kupona kabisa afya ya Papa Francisko."
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika Kusini CELAM
Kwa kuzingatia siku kuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro, kielelezo cha mamlaka aliyopewa na Kristo Yesu ili kufundisha, kuongoza na kuwatakatifu watu wa Mungu inayofanyika ifikapo tarehe 22 Februari ya kila mwaka, Kadinali Jaime Spengler, rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Brazil(CNBB) na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean(CELAM),alihimiza kuomba kwa ajili ya uponyaji wa Papa, huku akiongeza nia ya maombi wakati wa maadhimisho kwamba: âBwana Mungu, mtumishi wako, Papa Francisko, amekuwa kwetu âshuhuda wa mateso ya Kristo.â
Ulimwengu wa siasa unamtakia haueni Papa Francisko
Hata ulimwengu wa siasa umemtakia uponyaji haraka Papa Francisko, ambapo kwa mfano salamu za heri zimetoka kwa Rais wa Israel Isaac Herzog. Akizungumza katika Sinagogi la Roma, alimtakia ahueni ya haraka na kamili, huku âakikumbuka maneno yake muhimu ya kukemea chuki dhidi ya Wayahudi.â
Kiongozi wa Iran anamwombea Papa
Katika ujumbe kwenye X kutoka kwa Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian aliandika kuwa âNamuombea kwa Mwenyezi Mungu afya yake na apone haraka.â