Baba Mtakatifu amelala salama Hospitalini Gemelli
Papa Francisko aliyelazwa katika hospitali ya Roma tangu Februari 14,alilala salama na kuamka akafungua kinywa akiwa amekaa katika sofa.
Vatican News
Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imetoa sasisho asubuhi ya leo tarehe 20 Februari 2025 kuhusu hali halisi ya Baba Mtakatifu Francisko kuwa:
“Usiku ulipita kwa amani, Papa aliamka na kufungua kinywa akiwa ameketi katika sofa.”
Katika taarifa ya matibabu iliyotolewa jana jioni tarehe 19 Februari na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican iliakisi hali "zisizobadilika" na "kuboresha kidogo, hasa uvimbe " unaoneshwa na vipimo vya damu vilivyotathminiwa na wafanyakazi wa matibabu.
20 Februari 2025, 09:51