Papa katika Hospitali ya Gemelli:shida ya kupumua asubuhi
Papa Francisko,japokuwa alikuwa na maumivu zaidi kuliko jana lakini alitumia siku nzima kukaa kwenye kiti cha sofa.Kuwekewa damu ilikuwa ni muhimu na vipimo vinabaki kulindwa.
Vatican News
Kutoka katika Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican, ilitoa taarifa kuhusu matibabu juu ya Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi jioni tarehe 22 Februari 2025 kama ifuatavyo:
“Hali ya Baba Mtakatifu inaendelea kuwa tete. Kwa hiyo, kama ilivyokuwa imeelezwa jana, Papa hayuko nje ya hatari. Asubuhi ya leo, Papa Francisko alipata shida ya kupumua kama pumu ya nguvu ya muda mrefu, ambayo ilihitaji huduma ya oksijeni. Vipimo vya damu vya leo pia vilionesha anemia, inayohusishwa na upungufu wa damu, ambapo alihitaji kuwekewa damu. Baba Mtakatifu anaendelea kuwa macho na alitumia siku nzima akiwa amekaa katika sofa, hata kama alikuwa na maumvu kuliko jana. Kwa sasa, ubashiri bado umelindwa.”
22 Februari 2025, 21:19