MAP

Kanisa zima linaendelea kusali kwa ajili ya Papa Francisko. Kanisa zima linaendelea kusali kwa ajili ya Papa Francisko.  (AFP or licensors)

Kanisa la Italia kufunga na kusali kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia(CEI)Kardinali Zuppi ataongoza sala saa 2.00 usiku katika Kanisa la Mtakatifu Domenico huko Bologna:"Njia madhubuti ya kupyaisha ukaribu na upendo wa jumuiya za kikanisa za Italia."Sala hizo na misa zinaendelea katika makanisa yote mahalia kama vile Afrika na mabara mengine kwa ajili ya Papa Fransisko.

Vatican News

Katika Kanisa la Mtakatifu Dominiko huko Bolognga nchini Italia, Dominika tarehe 23 Februari 2025 Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu hilo na mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia(CEI), ataongoza Rosari Takatifu kwa ajili ya kuombea afya njema Baba Mtakatifu Francisko. Rosari Takatifu itafanyika saa 2.00 usiku masaa ya Ulaya ambapo ni saa 4 za Usiku masaa ya Afrika Mashariki na Kati. Kardinali Zuppi alisema: “Tunataka kuungana na Baba Mtakatifu, kumwomba Bwana amsaidie katika wakati huu wa mateso, ili apate nafuu na aweze kupona haraka iwezekanavyo. Itakuwa njia madhubuti ya kupyaisha ukaribu na mapenzi ya jumuiya za kikanisa za Italia, ambazo zimezidisha maombi yao kwa siku nyingi."

Usiku wa leo, kwa hakika, ni tukio la kwanza ambalo, kuanzia Bologna, litahusisha Makanisa yote nchini Italia, yakiungana pamoja, katika kukumbatiana kwa sala moja. Ofisi ya Baraza la Maaskofu kitaifa ya Liturujia inatayarisha vielelezo viwili, vinavyopatikana hivi karibuni, ili kusuka mlolongo huu wa sala unaokusanya jumuiya zote zinazomzunguka Askofu wa Roma anayesimamia Ushirika. Sala hiyo itaonesha mbashara kupitia Televisheni ya Baraza la Italia: TV2000 (Chaneli ya 28) na Play2000 (mtiririko wa Jukwaa la  streaming ya Tv2000  na  inBlu2000).

Kardinali Reina: Misa Maalum kwa ajili ya Papa

Dominika jioni, tarehe 23 Februari 2025 saa 11.30, jioni badala yake, Makamu wa Baba Mtakatifu Francisko wa Jimbo Kuu la Roma, Kardinali Baldassare Reina, ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano kwa maombezi ya pekee kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu, na huku akiomba mapadre na mapadre wa Parokia zote kufanya hivyo pia katika Maadhimisho yao  leo hii. Kardinali alitoa  mwaliko: "Napenda kuwaalika kujumuika kiroho katika Misa Takatifu nitakayoadhimisha jioni ya leo. Katika ushirika wa imani na sala, kila mmoja katika jumuiya yake tutainua sala zetu kwa Bwana kwa  ajili ya Baba Mtakatifu, ili aweze kumtegemeza kwa neema yake na kumjaza nguvu zinazohitajika ili kupitia wakati huu wa majaribu.

Kardinali Lojudice: Tumwombee Papa Fransisko

Sala kwa ajili ya afya ya Papa pia imeinuliwa kutoka katika  Makanisa dada ya Siena-Colle huko Val D'Elsa-Montalcino na Montepulciano-Chiusi-Pienza ambayo yanaendelea kusali katika kila jumuiya. Kwa mujibu wa Kardinali Augusto Paolo Lojudice, rais wa Baraza la Maaskofu wa Toscana alisema:  "Tunataka kumwonesha Papa  ukaribu wetu, upendo wetu na shukrani zetu. Umbo lake ni hatua muhimu na muhimu ya kumbukumbu kwa maisha yetu katika Kanisa wakati ambapo maadili ya Injili ni karibu kutengwa na maisha yetu ya kila siku: mshikamano, ukarimu, heshima ya maisha kwa namna zote.”  Kwa kuhitimisha Kardinali alieleza “ni ujitoaji wa kimwana wa waamini, pamoja na dhamira ya kuendelea kusali kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu.


Nchini Tanzania, Askofu Pisa,Rais wa TEC: Tumwombee Papa apone haraka na kabisa

Katika sala hiyo pia Kanisa Katoliki nchini Tanzania, kupitia Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Tanzania(TEC), alituma ujumbe kwa Kanisa lote kuungana pamoja katika Misa ya Dominika tarehe 23 Februari na siku sijazo kumuombe Baba Mtakatifu. Askofu Wolfgang Pisa,OFMCap, Askofu wa Jimbo la  Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) aliandika: “Kama mnavyofahamu Baba Mtakatifu wetu Fransisko alilazwa Gemelli Polyclinic, Roma tangu February 14th, 2025 kwa shida ya afya. Naomba tumkumbuke kwenye maadhimisho yetu ya Jumapili ya 7 ya Mwaka C,  kesho, Februari 23, au siku zitakazofuata. Kama Baraza la Maaskofu na Kanisa nzima la Tanzania kwa maombezi ya Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili msimamizi wa nchi yetu, tunamwombea Baba Mtakatifu Fransisko apone haraka na Kabisa.”

23 Februari 2025, 14:31