Maskofu Tanzania(TEC):Februari 23,Kanisa la Tanzania linasali kwa ajili ya Papa!
NIA KWA AJILI YA KUMWOMBEA BABA MTAKATIFU.
Kama mnavyofahamu Baba Mtakatifu wetu Fransisko alilazwa Gemelli Polyclinic, Roma tangu February 14th, 2025 kwa shida ya afya. Naomba tumkumbuke kwenye maadhimisho yetu ya Jumapili ya 7 ya Mwaka C, kesho, Februari 23, au siku zitakazofuata.
Kama Baraza la Maaskofu na Kanisa nzima la Tanzania kwa maombezi ya Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili msimamizi wa nchi yetu, tunamwombea Baba Mtakatifu Fransisko apone haraka na Kabisa.
+Wolfgang Pisa,OFMCap,Askofu wa Jimbo la Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC).
Ujumbe mwingi kutoka sehemu mbali mbali za Ulimwengu umefika kwa Papa kwa kumtakia matashi mema ya uponyaji na makanisa mengine duniani yanaendelea kusali kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko ili Mungu amjalie afya njema na kuendelea na utume wa kulichunga Kanisa lake.