Mkutano wa Rimini,wakati amani inakuwa na sura ya mama
Na Guglielmo Gallone – Rimini.
Binti yangu alikasirika sana, mnamo 2018, nilipomwambia nitajiunga na Jukwaa la Wazazi-Familia, shirika linalohamaisha mazungumzo kati ya familia za Wapalestina na Israeli ambao wamepoteza wapendwa wao kutokana na mzozo. Miaka kumi na sita kabla ya hapo, wakati wa vita ya Intifadha ya pili, mwanangu Qusay, mwenye umri wa miezi sita tu, alikufa mikononi mwangu. Nilikuwa nikijaribu kumwokoa na vita, lakini wanajeshi wa Israeli walinizuia. Baada ya tarehe 7 Oktoba 2023, maisha yetu yamezidi kuwa magumu. Wapalestina wote waliofanya kazi Israel wamepoteza kazi.
Hatuna malazi ya kutukinga na mabomu. Hatujui hata kinachoendelea kilomita chache kutoka hapo. Na watoto hawawezi tena kwenda shule, isipokuwa siku moja kwa Juma. Hivi karibuni, serikali ya Israeli pia imeunda vikwazo vipya: badala ya vituo vya ukaguzi vya kawaida, kuna vizuizi vinavyozuia kabisa kuzuguka. Katika hali ya dharura, tumetengwa. Hata hivyo, kila mwaka pamoja na Mzunguko wa Wazazi-Familia tunafanya adhimisho ambapo tunakumbuka wapendwa wetu wote na kutuma ujumbe kwa Ulimwengu kwamba: Waisraeli na Wapalestina wanaweza kusimama bega kwa bega. Kwa pamoja, tunaweza kufanya mabadiliko. Watoto wangu walipoona hotuba hiyo, walielewa kwa nini nilijiunga na shirika hilo. Binti yangu alinikumbatia. Kwa miaka mingi, nilipoteza imani yangu; kwa muda mrefu, binti yangu hakuelewa sababu na roho ya kujitolea kwangu, lakini hii ilikuwa matokeo muhimu zaidi, ambayo hufanya kila kitu kuwa kizuri zaidi, na rahisi zaidi.
Historia mbili za upatanisho na mazungumzo
Historia ya Layla al-Sheik, mama Mpalestina, ilisikika katika moyo wa ukumbi wa D3 wa Jukwaa la Rimini. Mkutano ulioandaliwa na Harakati ya ‘Comunione e Liberazione’ yaani ‘Ushirika na Ukombozi’ ndivyo ulianza. Na ukweli kwamba tukio la uzinduzi limejitolea kwa akina mama kwa ajili ya amani, kwa historia mbili za upatanisho na mazungumzo, ambazo husaidia kufahamu mara moja kiini cha siku hizi tano ambazo zinaongoza na kauli mbiu: “Katika maeneo ya majangwa, tutajenga kwa matofali mapya.†Layla hakuwa peke yake. Kando yake, katika jopo lililosimamiwa na mwandishi wa habari Alessandra Buzzetti, mwandishi wa TV2000 kutoka Nchi Takatifu, ni Elana Kaminka, Mwisraeli, mama wa Yannai, askari aliyeuawa mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Katika tarehe isiyoweza kufutika kwa hatima ya Mashariki ya Kati, Yannai aliokoa waajiri 80 na raia 20.
"Yannai alikuwa mwanangu, lakini kwangu alikuwa mwalimu," Elana alisema hayo katika maelezo yake. "Uongozi wake uliongozwa na hisia nyingi. Ya kwanza: kuwafanya wengine wahisi upendo wake ili wawe na ufanisi zaidi katika kuleta mabadiliko. Kisha, hisia ya wajibu. Kwangu mimi, Yannai ni mfano. Baada ya kumpoteza, nilihisi kama nimepoteza maisha yangu yote. Nilishindwa katika lengo kuu la kuwa mama: kumweka mtoto wake salama. Kisha, nilijiambia kwamba jambo pekee ambalo ningeweza kudhibiti lilikuwa itikio langu mwenyewe. Kwa hiyo, nilielewa mafundisho yake na kuanzisha mabadiliko mimi mwenyewe. Kwa hivyo nilijiunga na Mzunguko wa Wazazi."
Hisia ya Mipaka katika Nchi Takatifu
Leo,hii akina mama hawa wawili wanaishi umbali wa kilomita mbili tu: Layla huko Battir, Elana huko Tzur Hadssah. Hata hivyo, kwa Layla, hawezeka kuvuka mpaka huo. Lakini Elana, kwa ukakamavu na utunzaji ambao akina mama pekee wanaweza kuwa nao, hajawahi kukata tamaa kwa alisema: "Sisi ni akina mama. Tunaelekea kuwa vitendo. Layla ni jirani yangu kwa kila hali, lakini kama nisingemchukulia hivyo, maisha yangu yangekuwa magumu. Kwa kifupi, unahitaji majirani wema ili kuwa na maisha mazuri. Watu wenye msimamo mkali katika jamii yetu, hata hivyo, wanafikiri wanaweza kuwaondoa majirani zetu. Hili halitafanyika. Lakini tunahitaji kuelewa ni watu wangapi watalazimika kupoteza maisha kabla ya kila mtu kuelewa kwamba Waisraeli na Wapalestina wataishi hapa daima."
Scholz:"Wacha tulete upatanisho kwenye jangwa la vita."
Baada ya yote, huu ndio ujumbe uliowasilishwa na Bernard Scholz, rais wa Mfuko wa Mikutano hiyo ya Urafiki Kati ya Watu, katika hotuba yake ya ufunguzi alisema: “Tunaweza kuanza toleo hili la arobaini na sita kwa uchambuzi mbalimbali, lakini hakuna hata mmoja kati yake ambaye angeweza kukomboa uhuru wetu wa kuchukua hatua kwa mwanzo mpya. Kuanzia ambapo kila kitu kinaonekana kumalizika. Kichwa cha mkutano huu kinasema wazi kuwa jangwa zipo, lakini hata katika majangwa haya inawezekana kulima na kujenga pamoja. Katika uso wa kujiuzulu sana, tunataka kuleta lishe na urafiki kwenye jangwa la upweke uliopo, lakini juu ya yote, upatanisho kwenye jangwa la vita."
Ushuhuda wa Sr Aziza
Na hapa ndipo ushuhuda wa Azezet Habtezghi Kidane ulipokuja. Yeye ni mtawa wa Comboni wa Eritrea, anayejulikana pia kama Sista Aziza, ambaye alifanya kazi kwa miaka kadhaa huko Israeli na Wilaya za Palestina, kwanza Sudan na kisha Eritrea. Katika hotuba yake alieleza kuwa: "Kama Masista wa Comboni, lengo letu ni kujenga madaraja, hivyo tunawageukia wale wanaowajali walio hatarini zaidi. Miongoni mwao ni Wabeduini wa Jangwa la Yudea. Walituambia wana hofu kuu mbili: mustakabali wa watoto wao na ukosefu wa huduma za afya. Haya yote yanaleta chuki kubwa, ikichochewa na ukweli kwamba ukuta uliojengwa kati ya Waisraeli na Wapalestina unatutenganisha na kuonana usoni. Ndiyo maana mmoja anamuogopa mwenzake. Na kila mwaka kujitenga hii inakuwa ngumu zaidi. Lakini pamoja na vita na vurugu, hakuna matumaini. Kwa maana unapouona uso wa huyo mwingine, unamwona Mungu.â€
Vidonda visivyoweza kudumu, matumaini yasiyo na mwisho
Jeraha lililosababishwa na kifo cha mtoto, katika moyo wa mama, haliponi kamwe. Haya ni majangwa makubwa na yasiyopitika ya wale wanaoishi katika historia. Hata hivyo, wanawake hawa wawili leo hii walionesha kwamba njia nyingine isiyokuwa kulipiza kisasi na chuki inawezekana. Inahitaji unyenyekevu, ujasiri, na azimio. Lakini hawa ndio "wajenzi wa jumuiya, kuishi pamoja, amani, ushiriki na mshikamano," ambayo Rais wa Jamhuri ya Italia, Sergio Mattarella, alirejea katika ujumbe wake kwa Mkutano huo.
Jumuiya huharibika pale ambapo kutojihusisha au kutojali kunatawala. Kujenga, hata hivyo, kunamaanisha kujiweka tena kwenye njia ya historia. Na hili ndilo tunalolenga kufanya katika Mkutano ambao, saa baada ya saa, unaohuishwa na makabiliano, vijana wa kujitolea, watu binafsi, historia,na makongamano,vyote vinaakisi lengo la siku hizi, ambalo Papa Leo XIV alilibainisha na kulisisitiza katika salamu yake: “Hebu tufukuzwe jangwani na tuone sasa kile kinachoweza kuzaliwa kutoka kwenye vifusi na kutokana na mateso mengi sana, yasiyo na hatia.â€