UN:Waisraeli na Wapalestina lazima waruhusiwe kuishi bega kwa bega kwa amani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kauli ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk, kupitia wasifu wake wa X baada ya mwanga wa kijani kwa mpango wa Netanyahu, wa Serikali ya Israeli kutaka kumiliki Gaza inabainisha: “lazima usitishwe mara moja. unakwenda kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kwamba Israel lazima ikomeshe ukaliaji wake kwa mabavu haraka iwezekanavyo, kufikia muafaka wa suluhisho la Serikali mbili zilizokubaliwa na haki ya Wapalestina kujitawala."
Serikali ya Israeli inapaswa kuokoa maisha ya raia wa Gaza
Katika Ujumbe huo Kingozi wa UN anaandika kuwa: “Kwa ushahidi wote hadi sasa, ongezeko hili zaidi litasababisha watu wengi zaidi kulazimika kuyahama makazi yao, mauaji zaidi, mateso yasiyostahimilika zaidi, uharibifu usio na maana na uhalifu wa kikatili. Vita vya Gaza lazima viishe sasa. Na Waisraeli na Wapalestina lazima waruhusiwe kuishi bega kwa bega kwa amani. Badala ya kuzidisha vita hivi, Serikali ya Israel inapaswa kuweka juhudi zake zote katika kuokoa maisha ya raia wa Gaza kwa kuruhusu mtiririko kamili, usio na vikwazo wa misaada ya kibinadamu. Mateka hao lazima waachiliwe mara moja na bila masharti na makundi yenye silaha ya Palestina. Wapalestina wanaozuiliwa kiholela na Israel lazima pia waachiliwe mara moja na bila masharti.”