ÐÓMAPµ¼º½

Msako mkali unaendelea wakati Watu,akiwemo mmisionari wa Ireland na mtoto mlemavu walitekwa nyara huko Haiti. Msako mkali unaendelea wakati Watu,akiwemo mmisionari wa Ireland na mtoto mlemavu walitekwa nyara huko Haiti.  (ANSA)

Haiti:Watu Tisa Watekwa nyara,akiwemo mmisionari na Mtoto Mlemavu

Mtu mwenye silaha alishambulia Kituo cha watoto yatima cha Sainte-Hélène huko Kenscoff,kusini mashariki mwa mji mkuu Port-au-Prince,Haiti na kuwateka nyara mmisionari Gena Heraty wa Ireland,wafanyakazi saba na mtoto mwenye umri wa miaka mitatu mlemavu.Tukio hilo linakuja huku kukiwa na hali numu ya taasisi na utawala wa magenge yenye silaha.Kulingana na UN zaidi ya watu 1,500 waliuawa kati ya Aprili na Juni na mamia ya utekaji nyara na unyanyasaji wa kingono.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Watu tisa walitekwa nyara na kundi lililojihami ambalo lilivamia kituo cha watoto yatima huko kusini mwa mji mkuu wa Haiti usiku wa tarehe 4 Agosti 2025. Miongoni mwao walikuwa mmisionari wa Ireland Gena Heraty, ambaye amefanya kazi na shirika la "Nos Petits Frères et SÅ“urs" kwa zaidi ya miaka 30, wafanyakazi saba wa Haiti, na mtoto mwenye umri wa miaka mitatu mlemavu. Kulingana na vyanzo vya ndani, washambuliaji walivunja uzio na kuingia ndani ya jengo hilo bila kufyatua risasi. Mara tu baada ya shambulio hilo, walitishia kuwalazimisha mateka kuondoka kwenye jengo hilo kwa miguu. Polisi ambao waliingilia kati tu baada ya kengele kupigwa na wafanyakazi waliokuwa wamesalia ndani ya jengo hilo, walianzisha msako katika eneo hilo, lakini hadi bila matokeo. Na hakujakuwa na madai ya uwajibikaji au maombi ya fidia.

Msururu wa vurugu,Haiti

Tukio hili ni mfano mwingine wa Haiti iliyonaswa katika msururu wa vurugu. Mgogoro wa nchi hiyo ni matokeo ya ombwe la muda mrefu la mamlaka kufuatia mauaji ya Rais Jovenel Moïse mnamo 2021. Tangu 2024, mji mkuu, Port-au-Prince, umekuwa chini ya udhibiti wa magenge yenye silaha, na kumlazimisha Waziri Mkuu wa zamani Ariel Henry kujiuzulu na kusababisha kuundwa kwa Baraza la Rais wa Mpito, ambalo sasa linaongozwa na Waziri Mkuu wa muda Didier Fils-Aimé. Magenge yamepanua ushawishi wao zaidi ya mji mkuu, wakati polisi wa kitaifa, kwa idadi na uhaba wa vifaa, wanajitahidi kuhakikisha utulivu na usalama. Katika hali hii, taasisi zinazidi kutengwa, na idadi ya watu wanaishi chini ya tishio la mara kwa mara la vurugu, unyang'anyi, na utekaji nyara. Kwa sababu hizi, nchi nzima inakabiliwa na moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu.

Ripoti ya UN:hali ya Haiti inatia wasiwasi kwa haki za binadamu

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa, iliyotolewa kunako tarehe 2 Agosti 2025, inaonesha hali inayoelezwa kuwa ya kutia wasiwasi sana kwa haki za binadamu nchini Haiti: angalau watu 1,520 waliuawa na 609 kujeruhiwa kati ya Aprili na Juni 2025. Wengi wa waathirika walikuwa wamejilimbikizia mji mkuu, Port-au-Prince, lakini ripoti hiyo pia inabainisha ongezeko kubwa la vurugu katika idara za Bas-Arti-Arti.Mashambulizi yanaendelea kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kuzidisha janga la kibinadamu ambalo tayari limekithiri, na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao na athari kubwa, haswa kwa wanawake na watoto," Ulrika Richardson, Mwakilishi Maalum wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti.

Magenge ya kihalifu yapanua mashambulizi 

Mbali na vifo na majeruhi, ripoti hiyo inaandika angalau visa 185 vya utekaji nyara na visa 628 vya ukatili wa kijinsia, vingi vikiwa dhidi ya wanawake na watoto, na inakemea matukio ya utumwa, biashara haramu ya binadamu na unyanyasaji wa kingono. Mwishoni mwa Juni, kulikuwa na zaidi ya watu milioni 1.3 wakimbizi wa ndani kati ya watu takriban milioni 11. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, magenge ya wahalifu yamepanua na kuzidisha mashambulizi yao, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kufikia malengo yao na kuzidisha zaidi udhaifu wa mfumo wa kijamii.

05 Agosti 2025, 13:45