ĐÓMAPµĽş˝

Wapalestina wakisubiri kupokea chakula kutoka jiko la hisani,katika mji wa Gaza Wapalestina wakisubiri kupokea chakula kutoka jiko la hisani,katika mji wa Gaza 

Caritas Internationali na mashirika zaidi ya 100 ya kibinadamu yalaani ukosefu wa msaada Gaza!

Caritas Internationalis na mashirika zaidi ya 100 ya kibinadamu ambayo yanalaani vikali kwamba kuwasili kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza bado kunazuiwa.Mwezi Julai kipekee,maombi zaidi ya 60 yalikataliwa kwa sababu ya uhalali huu.Uzuizi huu umeacha chakula,dawa,maji na vifaa via makazi vyenye thamani ya mamilioni ya dola vikiwa vimekwama katika maghala yote Jordan na Misri,huku Wapalestina wakikabiliwa na njaa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Caritas Internationalis, pamoja na zaidi ya mashirika 100 ya kibinadamu, inalaani vikali uzuiaji unaoendelea wa misaada ya kibinadamu huko Gaza. Licha ya madai ya mamlaka ya Israel kwamba hakuna kikomo kwa misaada ya kibinadamu inayoingia Gaza, mashirika mengi makubwa ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yameshindwa kuwasilisha hata lori moja la vifaa via kuokoa maisha tangu tarehe 2 Machi. Badala ya kupunguza mrundikano wa bidhaa zinazoongezeka, mamlaka za Israeli zimekataa maombi kutoka kwa mashirika mengi yasiyo ya kiserikali kuleta bidhaa za kuokoa maisha, wakitaja kwamba mashirika haya “hayana mamlaka ya kutoa msaada.”

Mwezi Julai kipekee, maombi zaidi ya 60 yalikataliwa kwa sababu ya uhalali huu. Uzuizi huu umeacha chakula, dawa, maji na vifaa via makazi vyenye thamani ya mamilioni ya dola vikiwa vimekwama katika maghala kote Jordan na Misri, huku Wapalestina wakikabiliwa na njaa.“ Shirika la Anera lina zaidi ya dola milioni 7 za vifaa vya kuokoa maisha vilivyozuiwa kuingia Gaza, ikiwa ni pamoja na pallet 744 za mchele, zinazotosha milo milioni sita, zimezuiliwa huko Ashdod zikiwa umbali wa kilomita chache,” alisema Sean Carroll, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Anera. Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali sasa yaliambiwa kuwa hayana idhini ya kutoa misaada, lakini yamefanya kazi huko Gaza kwa miongo kadhaa, yanaaminika na jamii na uzoefu katika kutoa misaada kwa usalama. 

Kutengwa kwao kumeacha hospitali bila vifaa via msingi, watoto, watu wenye ulemavu, na wazee wakifa kutokana na njaa na magonjwa yanayoweza kuzuilika, na wafanyakazi wa misaada wenyewe kwenda kazini wakiwa na njaa. Uzuizi huu unahusishwa na sheria mpya za usajili za mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali (INGOs) zilizotangazwa mwezi Machi. Chini ya sheria hizi mpya, usajili unaweza kukataliwa kwa misingi ya vigezo visivyo wazi na via kisiasa, kama vile kudhoofisha uhalali wa taifa la Israeli. Mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali (INGOs) ziliona kuwa mchakato huo uliundwa ili kudhibiti mashirika huru, kunyamazisha utetezi, na kudhibiti ripoti za kibinadamu. Uzuiaji huu mpya wa ukiritimba hauendani na sheria ya kimataifa iliyoanzishwa kwani unaleta udhibiti wa Israel na unyakuzi wa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Maandalizi ya chakula kwa ajili ya watu wa Gaza
Maandalizi ya chakula kwa ajili ya watu wa Gaza   (AFP or licensors)

Leo hii, hofu za INGOs zimethibitisha ukweli, mfumo wa usajili sasa unatumika kuzuia zaidi misaada na kunyima chakula na dawa katikati ya hali mbaya zaidi ya njaa. “Tangu kuzingirwa kamili kulipotolewa tarehe 2 Machi, CARE imeshindwa kutoa hata kidogo  ya vifaa vyetu vilivyohifadhiwa vyenye thamani ya dola milioni 1.5 huko Gaza,” alisema Jolien Veldwijk, Mkurugenzi wa Nchi wa shirika la  CARE.  “Hii inajumuisha shehena muhimu za vifurushi via chakula, vifaa via matibabu, vifaa via usafi, vifaa via kutunza hadhi, vifaa via utunzaji wa mama na watoto wachanga. Jukumu letu ni kuokoa maisha, lakini kutokana na vikwazo via usajili, raia wanaachwa bila chakula, dawa na ulinzi wanaohitaji haraka.”

“Oxfam ina bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 2.5 ambazo zimekataliwa kuingia Gaza na Israel, hasa vifaa via WASH ikiwemo maji na usafi wa mazingira pamoja na usafi wa vyakula,” alisema Bushra Khalidi, Kiongozi wa Sera za Oxfam. “Mchakato huu wa usajili unatoa ishara kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kwamba uwezo wao wa kufanya kazi unaweza kugharimu uhuru wao na uwezo wa kujieleza.”

Vizuizi hivi ni sehemu ya mkakati mpana zaidi unaojumuisha kinachojulikana kama mpango wa “GHF” utaratibu wa usambazaji wa kijeshi unaohamasishwa kama suluhisho la kibinadamu.  Kiukweli, ni chombo muhimu cha kudhibiti, na Wapalestina wasiopungua 859 waliuawa karibu na maeneo ya “GHF” tangu kuanza kufanya kazi. “Mpango wa usambazaji wa chakula wa kijeshi umetumia njaa kama silaha na kuunda mateso. Usambazaji katika maeneo ya GHF umesababisha viwango via juu via ghasia na mauaji, hasa ya vijana wa kiume wa Kipalestina, lakini pia ya wanawake na watoto, ambao wamekwenda kwenye maeneo kwa matumaini ya kupokea chakula,” kulingana na Aitor Zabalgogeazkoa, mratibu wa dharura wa MSF huko Gaza.

Wapelestina wakijaribu kukumbia
Wapelestina wakijaribu kukumbia   (MAHMOUD ISSA)

kwa njia hiyo Wanatoa wito  kwa serikali zote na wafadhili: Waishinikize Israel kukomesha utumiaji wa msaada kama silaha, ikiwa ni pamoja na kupitia uzuiaji cha urasimu, kama vile taratibu za usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (INGOs); Wasisitiza kwamba, mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali INGOs yasishinikizwe kutoa taarifa nyeti za kibinafsi, kwa kukiuka Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR), au kuhatarisha usalama wa wafanyakazi au uhuru kama sharti la kutoa msaada. Wanadi kufunguliwa mara moja na bila masharti kwa njia zote za ardhi na kuweka mazingira ya kutoa misaada ya kibinadamu ya kuokoa maisha.

18 Agosti 2025, 10:08