ĐÓMAPµĽş˝

Kazi zenye suruba za kunyonya watoto na ngumu Kazi zenye suruba za kunyonya watoto na ngumu 

Siku ya kimataifa dhidi ya ajira za utotoni,Save the Children:Watoto wako hatarini

Katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Dhidi ya Ajira ya Watoto Shirika la Save the Children linasema jambo hili ni kubwa linalohatarisha haki za kimsingi za watoto,wasichana na vijana.Matatizo ya kiuchumi yanasukuma familia kuwategemea watoto wao ili kupata mapato ya ziada.Ukosefu wa Upatikanaji wa Elimu:Watoto wengi hasa wa vijijini hawapati elimu bora au shule.Unyonyaji kwa watoto wanaozamia nchi za kigeni bila kusindikizwa.

Angella Rwezaula – Vatican.

Ajira ya watoto ni jambo la kimataifa ambalo bado limeenea, mara nyingi limefichwa na ni vigumu kugundua, ambalo linahatarisha haki za msingi za mdogo, kuwanyima fursa ya kusoma, kukua kwa afya na kufurahia ustawi wa kimwili na kisaikolojia. Katika mkesha wa Siku ya Kimataifa Dhidi ya Ajira ya Watoto, ambayo itaadhimishwa tarehe 12 Juni 2025, Shirika la Save the Children, Saidia Watoto, limeibua dharura tena kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za utoto na ujana ambao pia Italia ni miongoni mwake kulingana na makadirio, watoto elfu 336 kati ya umri wa miaka 7 na 15 wanahusika katika uzoefu wa kuendelea, wa mara kwa mara au wa hapa na pale.

Kulingana na makadirio yaliyotolewa katika ripoti ya utafiti ya Save the Children iliyopewa jina: “Si mchezo”, 6.8% ya watoto walio na umri wa kati ya miaka 7 na 15 – karibu 1 kati ya 15 – wanahusika au wamehusika katika shughuli za ajira, lakini asilimia hiyo huongezeka miongoni mwa watoto wa miaka 14-15. Katika kundi hili la umri, kijana mmoja kati ya watano (20%), ameajiriwa na takriban mmoja kati ya watoto watatu wa umri wa miaka 14-15 (27.8%, takriban vijana 58,000) ana au amekuwa akijishughulisha na kazi ambayo inadhuru sana njia zao za elimu na ustawi wa kisaikolojia na kimwili kwa sababu inafanywa kwa kuendelea wakati wa shule au wakati wa usiku.

Ajira za utotoni
Ajira za utotoni

Sekta zilizo na matukio mengi zaidi ya utumikishwaji wa watoto ni upishi (25.9%) na mauzo ya rejareja katika maduka na shughuli za kibiashara (16.2%), lakini watoto wadogo pia wanafanya kazi mashambani (9.1%) au katika maeneo ya ujenzi (7.8%) na ripoti pia inaakisi aina mpya za ajira za  mtandaoni (5.7%). Ajira ya watoto huathiri njia za elimu: watoto wanaofanya kazi mara nyingi hufanya hivyo wakati wa saa za shule, na hivyo kusababisha kutokuwepo shuleni na muda mdogo wa masomo na shughuli nyingine za mafunzo, hivyo kuongeza hatari ya kuacha shule kabisa. Kuacha shule au kupata ujuzi duni pia kutakuwa na athari kwa hali ya kazi ya watoto wadogo, pamoja na hatari ya kukubali malipo ya chini, kazi za hatari kubwa katika siku zijazo, au ya kuongezeka kwa safu za NEET (vijana ambao hawasomi, kufanya kazi au wasiojumuishwa katika njia za mafunzo), katika mzunguko mbaya wa umaskini na ukosefu wa usawa.

Takwimuza  hivi karibuni  zaidi za Istat(nchini Italia) zimerekodi ongezeko la umaskini kamili wa watoto ambao, kwa kukosekana kwa uingiliaji uliolengwa, hatari ya kusababisha ongezeko zaidi la idadi ya wavulana na wasichana chini ya miaka 16 wanaohusika katika shughuli za kazi. Kwa sababu hii, Save the Children inasisitiza udharura wa kuchukua hatua katika nyanja mbalimbali, kutoka katika kupambana na umaskini wa kiuchumi hadi kusaidia utoaji wa elimu na mafunzo, pamoja na hatua ya harambee ya taasisi na wahusika wote wa kijamii na kiuchumi. Zaidi ya hayo, ni muhimu kulipa kipaumbele maalum kwa wanafunzi walio katika hali mbaya ya kijamii na kiuchumi, kutangaza habari zinazoenea kuhusu huduma na fursa zinazotolewa ili kuhakikisha haki ya elimu, kutoka katika ufadhili wa masomo hadi msamaha wa kodi, na kuhamasisha uanzishaji wa mipango ya usaidizi ya kibinafsi kwa wavulana na wasichana ambao wana hatari ya kukatiza taaluma yao ya shule kabla ya wakati.

Kazi za suruba za watoto
Kazi za suruba za watoto

"Nilifanya mambo ambayo yalikuwa ya kuchosha kwa msichana wa miaka 13 (...) unaweza kuifanya kwa siku chache lakini baada ya muda unachoka, huwezi kufanya hivyo. Ikiwa wewe ni mtu ambaye umezoa aina hii ya utaratibu, ndiyo, lakini baada ya muda unachoka, huna maisha ya kijamii, kwa maana ya kwamba huna marafiki, basi huwezi kufurahia, hivyo huwezi kufurahia. F., 17, ni kijana mmoja kutoka Palermo, Italia alisema. "Wanatumia kisingizio kwamba wewe ni kijana mdogo, kwamba lazima ujifunze - masaa mengi sana yanachosha na wakati mwingine mwili hauwezi kuvumilia" alimbuka kijana mwingine  wa miaka  19, kutoka Scalea.

Kwa watoto walio katika mazingira magumu zaidi, hatari ya kuishia katika mizunguko ya unyonyaji wa kazi ni kubwa zaidi. Kama ilivyokuwa kwa mtoto mdogo mwingine  wa kigeni ambaye hakusindikizwa  na mtu aliyewasili kutoka Tunisia: “Sikutaka kuomba pesa barabarani, kwa hiyo nililazimika kufanya kazi ili kupata pesa nilizohitaji. Nilikuwa nikikata mboga kwa ajili ya sandwiches za kebab, na kuosha sahani. Nilianza kuhudhuria shule ili kupata cheti cha shule ya Msingi lakini kazini waliniambia nisingeweza kwenda shule. Waliniambia kwamba ikiwa nitarudi shuleni tena, singeweza kufanya kazi nao. Pamoja na waelimishaji, basi nilielewa ni bora kuondoka na kuchukua kozi ya mafunzo. "

11 Juni 2025, 12:31