Italia/Afrika,Meloni:"Kwa muda mrefu Afrika imenyonywa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
"Ninatangaza kwamba tunafanya kazi katika mpango madhubuti wa kushughulikia suala la deni la mataifa ya Afrika, suala kuu kwa maendeleo ya bara ambalo, ikiwa halitashughulikiwa vya kutosha, linaweza kubatilisha juhudi zingine zote." Haya yalisemwa na Waziri Mkuu wa Italia Bi Giorgia Meloni, katika taarifa zake kwa waandishi wa habari kwenye mkutano wa kilele cha "Mpango wa Mattei kwa Afrika na Lango la Kimataifa: Juhudi za pamoja na Bara la Afrika,” uliofanyika Ijumaa tarehe 20 Juni 2025 Jijini Roma.
"Mpango ​​unapanga kubadilisha kiasi kizima cha deni kwa mataifa yaliyoendelea kidogo zaidi katika kipindi cha miaka 10 ijayo, kulingana na vigezo vya Benki ya Dunia, na kupunguza kwa 50% ya mataifa yenye mapato ya chini zaidi. Operesheni nzima katika miaka kumi itaturuhusu kubadilisha takriban euro milioni 235 za deni kuwa miradi ya maendeleo kutekelezwa ndani ya nchi,” alisema Waziri Mkuu.
Katika taarifa yake aidha aliongeza: “Tunaamini kwamba Afrika ni bara ambalo mustakabali wetu uko hatarini kuliko mahali pengine popote, na sisi Waitaliani na Ulaya kwa ujumla tumeitwa kuleta mabadiliko na tunaweza kuleta mabadiliko."
Kadhalika Bi Meloni alisema kuwa: "Changamoto mpya ni masimulizi kuhusu Afrika, ambayo kwa muda mrefu imenyonywa na kutumiwa. Ni bara tajiri sana ambalo leo hii linatoa fursa kubwa na linaweza kustaajabisha ikiwa litawekwa katika hali ya kuimarisha vitu vya ajabu ilivyo navyo."
"Mikataba iliyotiwa saini leo" katika mkutano wa kilele wa EU-Afrika "ina thamani ya bilioni 1.2 katika ahadi madhubuti. Zaidi ya hayo, "tunafanya kazi -katika mpango madhubuti wa deni la mataifa ya Afrika, suala ambalo lisiposhughulikiwa linahatarisha kubatilisha juhudi zetu zote. Tunaamini kuwa Afrika ni bara ambalo mustakabali wetu uko hatarini. Tunaamini kuwa kuimarisha Afrika kunamaanisha pia kuimarisha Ulaya, kujenga pamoja masharti ya utulivu wa pamoja." Bi Meloni aliwashukuru viongozi wote walioshiriki mkutano huo miongoni mwao alikuwapo hata hata Dr Philpo Mpango, Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Akili Nunde "ni teknolojia ya kimapinduzi" yenye "uwezo wa ajabu wa kubadilisha maisha, lakini kuna hatari kwamba itapanua mgawanyiko wa kidijitali kati ya wale wanaoimiliki na wale wasioweza. Sasa, Ulaya inafanya kazi na washirika ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaweza kushiriki katika mapinduzi ya AI: ni kuhusu ufikiaji. Na ndio maana Italia na Tume zimesaini tu makubaliano ya kufanya EU ijiunge na AI Hub kwa Maendeleo Endelevu."Hayo yalisemwa na Rais wa Kamisheni ya Tume ya Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, wakati wa huo wa kufunga mkutano wa kilele wa "Mpango wa Mattei kwa Afrika na Lango la Kimataifa: juhudi za pamoja na bara la Afrika" jijini Roma, ulioongozwa na Waziri Mkuu Giorgia Meloni na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa Afrika.
Mpango huo unaoongozwa na Italia, G7 na Umoja wa Mataifa "una mwelekeo mkubwa sana kwa Afrika", aliendelea von der Leyen. Tumejitolea kusaidia ukuaji wa ujuzi miongoni mwa wanasayansi wachanga wa Kiafrika na wajasiriamali. Tunawawezesha kwa nguvu ya kompyuta. Na kwa kweli, tuko wazi kwa ushirikiano na viwanda vyetu vya AI na, hivi karibuni, gigafactories, kuwapa wanaoanza fursa ya kujaribu na kutoa mafunzo kwa mifano yao kwenye viwanda vyetu vya AI."