Canada yaadhimisha Siku ya Kitaifa ya Watu Asilia
Na Kielce Gussie na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ndefu zaidi ya mwaka, wakati wa msimu wa kiangazi, huadhimisha Siku ya Kitaifa ya Watu wa Asili. Hizi ni Jumuiya za Mataifa ya Kwanza, Inuit, na Métis zinazosherehekea tamaduni, lugha na mila zao kwa wakati huu wa mwaka kwa vizazi. Kwa hiyo majira ya kiangazi yana umuhimu wa kina wa kiutamaduni na kiroho kwao kwani inaashiria wakati kwa kupyaisha uhusiano na kusherehekea.
Sherehe karibu na Canada
Nchini Canada, sherehe hutoa matukio haya ili kuonesha na kupiga mbizi zaidi katika historia na mila na tamaduni za Mataifa mbalimbali ya Kwanza na Watu wa Asili. Huko Montreal, jumuiya ya Mohawk ya Kahnawake iliandaa shughuli na warsha mbalimbali, ikiwa ni pamoja na onesho la kujaza samaki, warsha ya kutengeneza mambo ya kiutamaduni na tamasha la bure na wasanii wa Asili.
Miaka 10 ya kazi
Mwaka huu, 2025, ni kumbukumbu ya miaka 10 ya ripoti ya Tume ya Ukweli na Upatanisho ya Canada inayofichua urithi wa uharibifu wa shule za Bweni nchini Canada; na maadhimisho ya miaka sita ya ripoti ya Uchunguzi wa Kitaifa wa Wanawake na Wasichana wa Asilia waliotoweka na waliouawa. Papa Francisko alipotembelea nchini Canada mnamo Julai 2022, katika hotuba yake ya kwanza ya hadhara ilijumuisha kuomba radhi kwa wawakilishi wa Wenyeji wa Mataifa ya Kwanza, Métis, na Inuit kwa maovu yaliyofanywa na Wakristo wengi dhidi ya watu wa asilia wa Canada katika mfumo wa shule za bweni.
"Nimekuja katika nchi zenu za asili ili kuwaambia binafsi huzuni yangu, kumwomba Mungu msamaha, uponyaji na upatanisho, kueleza ukaribu wangu na kuomba pamoja nanyi na kwa ajili yenu," alisema Papa wakati ule. Kwa hiyo Siku ya Kitaifa ya Watu wa Asili imejitolea pia kuwakumbuka waathiriwa na familia zao zilizoathiriwa na historia ya mateso.
"Watu wa asili ni baraka"
Siku mbili kabla ya Siku ya Kitaifa, Mkutano wa Maaskofu wa Kikatoliki wa Kanada (CCCB) ulitoa taarifa kwa Kifaransa na Kiingereza, na kuwahimiza watu "kukumbuka na kutafakari juu ya urithi wa Papa Francisko na kutoa shukrani kwa maendeleo yaliyopatikana kuelekea upatanisho kwa miaka mingi." Katika taarifa yao Maaskofu hao wanasisitiza kuwa "Watu wa asili ni baraka kwa Kanisa na jamii ya Canada." Wanahimiza kila mtu kufungua mioyo na akili yake kwa kaka na dada zake na kuongeza uelewa wao juu ya Watu wa Asili, wakiwakumbusha Wakatoliki kwamba, kama "washiriki wa Kanisa, tunaitwa kujenga uhusiano unaosimikwa katika ukweli, haki na huruma." Walihitimisha kwa kuwaalika kila mmoja kuendelea na safari ya kutembea pamoja "katika roho ya matumaini na mshikamano kuelekea upatanisho."
Karibu miaka 30 ya historia
Mnamo 1996, Gavana Mkuu wa 25 wa Canada, Roméo LeBlanc alitangaza Juni 21 kama "Siku ya Kitaifa ya Watu wa Asili "kila mwaka. Uamuzi huo ulikuja baada ya miaka mingi ya mashauriano na kauli za kuungwa mkono na vikundi mbalimbali vya watu asilia kwa ajili ya kuunda siku hiyo. Mnamo 1982, Jumuiya ya Kitaifa ya Udugu wa Kihindi, ambayo sasa inaitwa Bunge la Mataifa ya Kwanza, ilitoa wito wa kuundwa kwa Siku ya Kitaifa ya Mshikamano wa Watu wa Asili. Miaka kumi na tatu baadaye, Bunge yaani mkutano wa kitaifa wa watu wa kiasili na wasio wa kiasili uliitisha siku kuu ya kitaifa ili kusherehekea kazi na michango ya watu wa kiasilia. Mnamo 1995, Tume ya Kifalme ya Watu wa asilia ilipendekeza kuundwa kwa Siku ya Kitaifa ya Watu wa Kwanza. Mnamo 2017, Waziri Mkuu Justin Trudeau wa cnhi hiyo alitangaza uamuzi wa kubadilisha siku hiyo kuwa "Siku ya Kitaifa ya Watu wa Asili."