Senegal,amani ya kijamii iliyotiwa saini ili kufufua bahati ya nchi
Vatican News
Nchini Senegal, serikali, vyama 24 vya wafanyakazi na mashirika 4 ya waajiri yametia saini makubaliano ambayo yanalenga kuhakikisha amani ya kijamii inadumu, ambayo nchi hiyo ya Afrika Magharibi inaihitaji sana. Mkataba huo - uliotiwa saini kiishara kunako tarehe 1 Mei 2025 katika Siku ya Wafanyakazi na inatoa usitishaji wa miaka mitatu wa mgomo, ambao unapaswa kumruhusu Rais Bassirou Diomaye Faye kuunganisha uchumi wa taifa linalokabiliwa na mzozo mkubwa wa kifedha na deni la umma ambalo linapaswa kufikia zaidi ya dola bilioni 7.
Kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi
Faye ili kukabiliana na hali hiyo mbaya, ametangaza kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha kwa utawala wa umma pamoja na upunguzaji mkubwa wa ajira, lakini rais mwenyewe ameweka bayana kuwa anataka kutekeleza miradi mikubwa zaidi ya ufufuaji inayohitaji muda zaidi na mshikamano wa kijamii usiojumuisha migongano na migomo. "Kujenga uchumi imara na shirikishi ambao utaturuhusu kugawanya tena mali. Na hatuwezi kufanya hivyo kwa kusimamia masuala ya kijamii," Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko alisema.
Idhini ya kijamii
Amani ya kijamii iliyopatikana na serikali, kulingana na kura za maoni ya umma, itathaminiwa na wananchi wengi ambao, hata hivyo, wana wasiwasi kuhusu ajira ndogo, gharama kubwa ya maisha na hali mbaya ya mfumo wa afya wa kitaifa. Msenegali huyo atahusika katika mchakato wa uimarishaji wa kiuchumi na kisiasa wa taifa hilo kupitia jukwaa la mtandaoni ambapo maswali 19 yataulizwa kuhusu demokrasia, uhuru na haki za binadamu, mchakato wa uchaguzi, mageuzi ya kitaasisi na usimamizi wa uchaguzi.