ÐÓMAPµ¼º½

Kimbunga Chido kilichopiga Msumbiji kiliongeza dharura zaidi zilizokuwapo. Kimbunga Chido kilichopiga Msumbiji kiliongeza dharura zaidi zilizokuwapo. 

Msumbiji:kuna mgogoro wa kibinadamu wa kutisha

UNHCR yatoa tahadhari kuwa bila fedha,rasilimali zimepunguzwa hadi kikomo.Katika nchi hiyo ya Kiafrika,iliyopigwa magoti na vita na hali mbaya ya tabianchi zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao wako hatarini kuachwa bila msaada.

Vatican News

Katika majuma machache tu, zaidi ya watu 25,000 wamelazimika kuacha makazi yao nchini Msumbiji. Hii ni dharura mpya ambayo inaongeza wale ambao tayari wamelazimika kukimbia kutokana na migogoro ya silaha, vimbunga na ukame. Huku ufadhili muhimu ukimalizika, UNHCR, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, na wahusika wengine wa masuala ya kibinadamu wanapiga kelele, huku uwezo wao wa kulinda na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wa dharura ukiongezwa hadi kikomo.

Kitovu cha mgogoro

Mkoa wa Cabo Delgado, wenye hifadhi kuu za gesi na maliasili nyingine za thamani kama vile vito na madini, sio tu msingi wa makampuni ya kimataifa, lakini pia ni kitovu cha mzozo unaoendelea ambapo wakimbizi wa ndani wanaongezeka. Mashambulizi ya vikundi visivyo vya serikali dhidi ya raia na miundombinu yanaendelea, na kusababisha uhamishaji wa watu kuendelea. Hata maeneo ambayo hapo awali yalichukuliwa kuwa tulivu, kama vile Ancuabe na Montepuez, yameathiriwa na mapigano na kulazimishwa kuhama wakaaji wao.

Dharura ya kibinadamu

Maendeleo haya yanakuja wakati wa mvutano mkubwa wa mwitikio wa kibinadamu nchini Msumbiji. Katika sekta zote, mashirika yanajitahidi kushuka kwa bajeti, wakati mahitaji yanaendelea kuongezeka. Matokeo yake ni mlingano hatari: ufadhili kidogo na watu wengi wanaohitaji. Msumbiji inakabiliana kwa wakati mmoja na mgogoro mara tatu: migogoro ya silaha na watu wanaosonga mbele, matukio ya hali ya tabianchi ya  mara kwa mara, na miezi ya machafuko ya baada ya uchaguzi.  Mnamo Machi, Kimbunga Jude kilipiga mkoa wa Nampula, na kuashiria kimbunga cha tatu kikubwa kupiga nchi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu pekee. Dhoruba hizi ziliharibu maeneo ambayo familia zilizohamishwa na mzozo wa silaha zilikuwa zimekimbilia, na kuzidisha mahitaji makubwa ya kibinadamu tayari.

Mgogoro wa kikanda

Hapo awali, machafuko ya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa 2024 yalisababisha baadhi ya raia wa Msumbiji kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Malawi. Wengi wao wamerejea kwa hiari, na kufanya idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu kufikia zaidi ya milioni 5. Mahitaji ya wakimbizi ni makubwa, kuanzia na usaidizi wa kimatibabu na kisaikolojia kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia. UNHCR pia ina wasiwasi kuhusu athari za kupunguzwa kwa ufadhili kwa mwitikio wa kibinadamu kwa wakimbizi. Hadi sasa, ni asilimia 32 tu ya dola milioni 42.7 zilizoombwa zimefika na Msumbiji inawahifadhi wakimbizi na waomba hifadhi karibu 25,000, hasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dhoruba kamili


Serikali na watu wa Msumbiji - linaelezea shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi - daima wameonyesha kujitolea kuwahifadhi na kusaidia wakimbizi na wakimbizi wa ndani, licha ya nchi hiyo kuwa mojawapo ya maskini zaidi duniani. Bei za vyakula, ambazo tayari ni za juu sana, zimepanda zaidi katika miezi ya hivi karibuni, mara nyingi kwa 10-20%, wakati mapato ya watu yanaendelea kupungua na kiwango cha juu cha deni la umma kinapunguza uwezo wa serikali kuingilia kati. Dhoruba kamili inakaribia, inalaani UNHCR, ambayo inahofia kuzorota kwa hali ya dharura ikiwa misaada ya kibinadamu ingekoma.
 

26 Mei 2025, 12:28