ÐÓMAPµ¼º½

2025.02.18 Musawah 2025.02.18 Musawah 

Toleo la 42 la Tuzo ya Amani la Niwano kwa Musawah,Mtandao wa Usawa katika Ulimwengu wa Kiislamu

Jumuiya ya kimataifa iliyoanzishwa nchini Malaysia imetambuliwa kwa kujitolea kwake kuwezesha uongozi wa wanawake katika uharakati wa kijamii,kisheria na kiroho, kukuza ushiriki wa kiraia,haki za binadamu na amani.Sherehe ya uwasilishaji itafanyika Tokyo mnamo tarehe 14 Mei 2025.

Vatican News

Toleo la 42 la Tuzo ya Amani la Niwano imetunukiwa tarehe 18 Februari 2025, kwa Harakati la kimataifa la Musawah, lililoanzishwa mnamo mwaka 2009 nchini Malaysia na kuendeshwa na wanawake wa Kiislamu, kwa kutambua dhamira yake kubwa ya kuimarisha uraia na kuishi pamoja kwa amani katika jamii mbalimbali na kuunda mazingira na majukwaa ya mazungumzo na mshikamano wa kidini. Kwa hivyo, Mfuko wa  Amani wa Niwano unaheshimu dhamira ya Musawah ya kuwezesha uongozi wa wanawake katika uharakati wa kijamii, kisheria na kiroho, kukuza ushiriki wa raia, haki za binadamu na amani.

Wafadhilii kutoka duniani kote

Musawah, mtandao wa Harakati ya  kimataifa ulioanzishwa mwaka wa 2009, unaohamaisha na kuthamini uhusiano unaozingatia uaminifu, heshima, utunzaji, haki na usawa. Unashughulikia ubaguzi wa kijamii na kiuchumi, kisheria na kisiasa kulingana na jinsia. Lengo la mtandao huo ni kufichua sauti za wanawake ambao wamenyamazishwa kwa muda mrefu katika jamii za kiutamaduni na kidini. Mtandao wake wa kimataifa unajumuisha mamia ya wafuasi kutoka Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na Kaskazini mwa Ulimwengu katika zaidi ya nchi 40, ambao wanapigania kila siku mabadiliko chanya katika mitazamo, desturi, sheria na sera kuunga mkono haki za binadamu za wanawake na wasichana katika nchi za Kiislamu. Vikundi vya washirika na wafuasi katika mtandao wa Musawah vinajitegemea lakini vina maono ya pamoja ya maendeleo ya wanawake, haki za binadamu na amani. Wengi wa washirika hawa wanatoka Afghanistan, Misri, Gambia, Indonesia, Jordan, Malaysia, Morocco, India, Pakistan, Uturuki, Sudan, Uganda. Washirika wa Musawah pia wamejitolea kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia.

Semina na kozi za mafunzo ili kuongeza uelewa miongoni mwa wanawake

Kwa ajili hiyo, semina na kozi za mafunzo zinahamaishwa kwa wanawake ili kuwasaidia kupambana na ukatili wa kijinsia na kuongeza rasilimali za kiuchumi ili kuwalinda ndani ya jamii zao. Aidha, vijana wanaelimishwa juu ya matumizi bora ya teknolojia, mitandao ya kijamii na jinsi ya kutetea mabadiliko ya kijamii. Wafuasi wa ndani wa Harakati la Musawah hushirikiana mwaka mzima ili kuimarisha ushirikiano wao na kuboresha hali ya wanawake duniani kote. Maandishi ya Musawah yanayotumika katika vyuo vikuu zaidi ya 30 ulimwenguni kote. Na ili kuwezesha na kuunga mkono sauti za wanawake wa Kiislamu katika jamii zao dhidi ya tafsiri ya kijinsia ya Kurani, na vita vyao dhidi ya sheria na desturi zinazokiuka haki zao, Musawah ametengeneza kwa miaka mingi maandishi mengi yaliyotumiwa katika vyuo vikuu zaidi ya 30 pia katika Umoja wa Mataifa (UN) na vile vile katika nyanja za mashirika mengi yasiyo ya kiserikali. Maandishi hayo yanatokana na yale yaliyoandikwa katika Koran na yanahoji kwamba kile kinachowasilishwa leo kama "sheria ya Kiislamu" si chochote zaidi ya tafsiri ya maandishi yaliyofanywa na watu wa zamani kulingana na maadili na kanuni za wakati wao. Sherehe ya uwasilishaji wa tuzo itafanyika Tokyo, Japan, Jumatano, tarehe 14  Mei 2025. Mbali na gombo la tuzo, Musawah itapokea medali na Yen yenye thamani ya milioni ishirini.

18 Februari 2025, 14:24