Vatican:Wanawake wa kiasili wanapaswa kuwa wahusika wakuu wa maisha bora ya baadaye
Vatican News
Wanawake wa kiasili hawapaswi kuonekana kama wanufaika wa sera za nje, bali kama wahusika wakuu katika kujenga siku zijazo, kukuza tamaduni za kiasili, kufuata njia zinazofaa za kiroho, na kuzingatia mila na lugha za watu wao. Ndiyo wazo kuu ambalo Vatican imetaka, kupitia Mwakilishi wake wa kudumu katika Shirika la Nchi za Marekani (OAS), Monsinyo Juan Antonio Cruz Serrano, ambaye alizungumza tarehe 13 Agosti 2025 mjini Washington katika Kikao Maalum cha Baraza la Kudumu la Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asilia Duniani na Juma la Nane kati ya Waamerika na Watu wa Asili Ulimwenguni kwa kuongozwa na mada: "sauti ya Wanawake Asilia: Mwonekano, Uongozi, Haki, na Uhuru wa Kiuchumi."
Mchango Mkubwa wa Wanawake katika Amazonia
Mwanadiplomasia huyo wa Vatican alikihakishia ukaribu wake “na watu wa kiasili na hasa wanawake” ili haki zao msingi ziweze kukuzwa na kulindwa. Alikumbuka, kama Papa Francisko alivyoandika katika Waraka wa Kitume Querida Amazonía, kwamba "katika Amazonia, kuna jumuiya ambazo zimejiendeleza [...] kutokana na uwepo wa wanawake wenye nguvu na wakarimu." Jumuiya ambazo zingeporomoka "kama wanawake wasingekuwepo, kuwaunga mkono, kuwalisha, na kuwatunza. Hii inaonyesha uwezo wao wa kipekee."
Ahadi ya Kanisa
Kanisa Katoliki, pamoja na taasisi na kazi zake, linajali watu wa kiasili katika sehemu nyingi za ulimwengu, Askofu Mkuu Cruz Serrano kisha alibainisha, "kuwekeza katika elimu na afya zao na kuongeza ufahamu katika jamii" ili watu hawa "waweze kuwa wahusika wakuu na viongozi wa historia yao wenyewe." "Ili kufikia lengo hili," mabaraza kadhaa ya kikanisa "yanafanya kazi kwa bidii, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya maaskofu, majimbo, mabalozi wa kitume, katika maeneo, vikarieti, parokia, misheni na Mtandao wa Kanisa wa Amazonia (REPAM)."
Msaada wa Vatican kwa programu kwa watu wa kiasili
Hatimaye, kufanya upya uungwaji mkono wa Vatican kwa ajili ya mipango inayolenga kukuza sauti ya watu wa kiasilia na kulinda haki zao na kuhakikisha ushiriki wao kamili katika maisha ya jamii," mwakilishi wa kudumu wa Vatican alitoa sifa kwa kazi ya Umoja wa Mataifa ya Marekani kwa niaba ya watu wa kiasilia na watu walio hatarini, wakiwemo wanawake na wasichana."