Msamaha "bila makadirio"
Andrea Tornielli
"Msamaha wa kweli haungojei toba, bali hujitoa kwanza, kama zawadi ya bure, hata kabla ya kupokelewa." Kwa maneno haya, Papa Leo XIV alitoa maoni yake juu ya kifungu cha Injili ya Yohane kinachoeleza Yesu akimtolea tonge la mkate Yuda msaliti. Ni mantiki ya kimungu iliyo mbali na ile ya kibinadamu ya do ut des, (sentesi ya kilatini yanye maana “ninatoa ili nawe upate kutoa.” Papa alielezea kuwa Yesu, si kwamba hajuhi kinachotokea, lakini kwa usahihi kwa sababu anaona wazi, anajua kwamba "uhuru wa wengine, hata wakati unapopotea katika uovu, bado unaweza kufikiwa na mwanga wa ishara ya upole." Hii ni kashfa ya msamaha wa "kuzuia", ambayo inatarajiwa, na utoaji wa kukumbatia kwa huruma bila kuhitaji masharti yoyote. Kama ilivyotokea kwa Zakayo mtoza ushuru, ambaye alitubu kwa sababu alikuwa ameitwa na kukaribishwa na Yesu, ambaye alikuwa amejikaribisha nyumbani kwake, kwa kufadhaika kwa kila mtu kitendo cha Mnazareti cha kuvunja mapokeo na mkusanyiko.
Ni kiasi gani maisha yetu na mahusiano yetu yanahitaji msamaha huu. Ni kiasi gani ulimwengu wetu unahitaji msamaha huu, ambao "sio kusahau, sio udhaifu." Maneno ya kinabii yanayokumbukwa ya ujumbe wa Siku ya Amani Ulimwengu mwaka 2002, ambayo Mtakatifu Yohane Paulo II alichapisha muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la kunako Septemba 11 huko Marekani. Wakati kila mtu akifikiria juu ya vita vya "kuzuia", kutokana na ukubwa wa shambulio hilo, Papa alitaka kusema: "Hakuna amani bila haki, hakuna haki bila msamaha." "Mara nyingi," Papa Wojtyla alisema, "nimetulia kutafakari juu ya swali: ni njia gani inayoongoza kwenye urejesho kamili wa utaratibu wa kimaadili na kijamii uliokiukwa kikatili? Usadikisho, ambao nimeufikia kwa kutafakari na kujihusisha na Ufunuo wa kibiblia, ni kwamba utaratibu uliovunjika hauwezi kurejeshwa kikamilifu isipokuwa haki na msamaha vikiunganishwa. Nguzo za amani ya kweli ni haki na aina hiyo maalum ya upendo ambayo ni msamaha." Sio watu binafsi pekee, bali pia "familia, vikundi, majimbo, na jumuiya ya kimataifa yenyewe, wanahitaji kuwa wazi kwa msamaha ili kuanzisha tena vifungo vilivyovunjika, kuondokana na hali ya kulaaniwa kwa kila mmoja, na kuondokana na kishawishi cha kuwatenga wengine kwa kuwanyima uwezekano wa kukata rufaa. Uwezo wa msamaha ndio msingi wa kila mpango kwa jamii ya siku za usoni yenye haki zaidi na inayounga mkono."
Kushindwa kusamehe, hata hivyo, Mtakatifu Yohane Paulo II alieleza, "hasa inapochochea kuendelea kwa migogoro, kuna gharama kubwa kwa maendeleo ya watu. Rasilimali hutumiwa kusaidia mbio za silaha, gharama za vita, na matokeo ya kulipiza kisasi kiuchumi. Hivyo, rasilimali fedha zinazohitajika kuzalisha maendeleo, amani na haki hazipo. Ni kiasi gani Ubinadamu unakabiliwa na maumivu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupatanisha, ni kiasi gani uvumilivu kuchelewa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kusamehe! Amani ni sharti la maendeleo, lakini amani ya kweli hupatikana kwa msamaha tu.
Papa Leo XIV katika Katekesi yake alieleza kuwa "bila msamaha hakutakuwa na amani kamwe!" Na alitualika kwenye siku ya maombi na kufunga kwa ajili ya amani siku ya Ijumaa, tarehe 22 Agosti ili kuomba maombezi ya Maria, Malkia wa Amani, na kumwomba Mungu amani na haki kwa ulimwengu unaokumbwa na vita. Kwa ulimwengu wetu, ambao unahitaji sana msamaha wa "kinga".