Kutoka Ulaya na ulimwengu,Tor Vergata inajazwa na matarajio ya kumuona Papa Leo XIV
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Saa 4:30 asubuhi, "vijana bora" wa Papa Leo XIV wamepangwa na tayari wakijaza uwanja mkubwa wa Tor Vergata. Nafasi nzuri zaidi, ambazo anaweza kuonekana Papa zaidi tayari zimekaliwa. Mahujaji hao vijana ambao kwa sasa wanashiriki Jubilei ya Vijana, bado watasubiri kwa saa nyingi kabla ya kukutana na Papa kwenye mkesha wao leo hii 2:30 usiku, ambazo ni saa 3.30 masaa ya Afrika Mashariki na Kati. Kisha watalala hapo hapo katika mifuko yao ya kulalia, na watahudhuria Misa Takatifu Dominka tarehe 3 Agosti 2025, saa 3.00 kamili asubuhi masaa ya Ulaya na saa 4 masaa ya Afrika Mashariki na Kati.
Wengi wao walifika kwa njia ya chini ya ardhi (Metropolitan) hadi kituo cha Anagnina. Kwa kukosa subira, kutoka hapa, walipeperusha bendera zao za kitaifa, huku wakaimba nyimbo zao za kitaifa, wakasali sala zao, na kuchezea fulana za rangi za "mahujaji wa matumaini." Kisha, chini ya jua la Roma la mwezi Agosti, ambalo tayari lilikuwa kali tangu asubuhi na mapema, waliondoka kwenda Tor Vergata, kwa mabasi au kwa miguu.
Njia ya Schiavonetti, njia ndefu inayoelekea kwenye kituo kikuu cha ununuzi cha kitongoji hicho, leo hakijajazwa na magari yanayopanga foleni kwa kawaidi kwa ajili ya ununuzi wa Jumamosi, bali na kundi la vijana wanaosafiri, wakiwa wamejihami kwa mikeka ya kambi, kofia, bendera, tarumbeta na ngoma.
Mizinga ya maji inayonyunyizia maji baridi, iliyowekwa kando ya njia, inatoa kiburudisho cha kuburudisha kwa matembezi yao. Wakati hatimaye wataona uwanja mkubwa sana kwa hatua kubwa, ambapo Papa atasali na kuumega mkate wa Ekaristi pamoja nao, na hivyohawawezi kujizuia kutoa kilio cha kitulizo na furaha!
Kwenye uwanja mkubwa sana wa Tor Vergata, mawazo yao yanaenda kasi ili kuunda njia bora zaidi, kwa ajili yao na kundi lao. Turuba na miavuli zimefungwa kwenye vikwazo ili kutoa kivuli kikubwa iwezekanavyo. Taulo za ufukweni, miwani ya jua, na mafuta mengi ya kujikinga na jua: baadhi ya watu wamelala kwenye jua, wakipitisha muda.
Mabango yenye majina ya majimbo yao, jiji lao, kikundi chao cha parokia, jumuiya yao ya kiroho ni vitu vya mpito, na mablanket, ambazo zinawaweka pamoja katika nafasi hii ya ajabu na isiyo na mipaka, kati ya Tanga la Calatrava na milima ya Castelli Romani: wanasaidia vijana hawa sana, wengine labda kuwa na uzoefu wao kwa mara ya kwanza kuwa mbali na wazazi wao, ili kujisikia karibu kidogo na nyumbani.