杏MAP导航

Tafuta

Vijana wanatarajia kumuona Papa Leo XIV katika Mkesha wa Jubilei ya vijana, huko Tor Vergata, in Roma. Vijana wanatarajia kumuona Papa Leo XIV katika Mkesha wa Jubilei ya vijana, huko Tor Vergata, in Roma. 

Kutoka Ulaya na ulimwengu,Tor Vergata inajazwa na matarajio ya kumuona Papa Leo XIV

Tangu asubuhi,mto wa vijana wa kiume na wa kike kutoka mabara matano umekuwa ukijaza eneo kubwa sana ambapo,jioni,tukio muhimu la Jubilei ya Vijana litafanyika:mkesha na Papa,ambaye ataadhimisha Misa katika eneo hilo asubuhi tarehe 3 Agosti 2025.Mahema,mifuko ya kulalia,bendera,mabango na mikeka vimetawanyika katika sekta mbalimbali.Mamia ya maelfu ya mahujaji wamehudhuria,wakiwa na hamu kubwa ya kushiriki imani yao na matumaini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Saa 4:30 asubuhi, "vijana bora" wa Papa Leo XIV wamepangwa na tayari wakijaza uwanja mkubwa wa Tor Vergata. Nafasi nzuri  zaidi, ambazo  anaweza kuonekana Papa zaidi tayari zimekaliwa. Mahujaji hao vijana ambao kwa sasa wanashiriki Jubilei ya Vijana, bado watasubiri kwa saa nyingi kabla ya kukutana na Papa kwenye mkesha wao leo hii  2:30 usiku, ambazo ni saa 3.30 masaa ya Afrika Mashariki na Kati. Kisha watalala hapo hapo katika mifuko yao ya kulalia, na watahudhuria Misa Takatifu Dominka tarehe 3  Agosti  2025,  saa 3.00 kamili  asubuhi masaa ya Ulaya na saa 4 masaa ya Afrika Mashariki na Kati.

Furaha ya vijana kujiandalia mkesha
Furaha ya vijana kujiandalia mkesha   (MATTEO CIAMBELLI)

Wengi wao walifika kwa njia ya chini ya ardhi (Metropolitan) hadi kituo cha Anagnina. Kwa kukosa subira, kutoka hapa, walipeperusha bendera zao za kitaifa, huku wakaimba nyimbo zao za kitaifa, wakasali sala zao, na kuchezea fulana za rangi za "mahujaji wa matumaini." Kisha, chini ya jua la Roma la mwezi Agosti, ambalo tayari lilikuwa kali tangu asubuhi na mapema, waliondoka kwenda Tor Vergata, kwa mabasi au kwa miguu.

Vijana wameanza kujiandaa na mkesha
Vijana wameanza kujiandaa na mkesha   (MATTEO CIAMBELLI)

Njia ya  Schiavonetti, njia ndefu inayoelekea kwenye kituo kikuu cha ununuzi cha kitongoji hicho, leo hakijajazwa na magari yanayopanga foleni kwa kawaidi kwa  ajili ya ununuzi wa Jumamosi, bali na kundi la vijana wanaosafiri, wakiwa wamejihami kwa mikeka ya kambi, kofia, bendera, tarumbeta na ngoma.

Maandalizi wa Mkesha
Maandalizi wa Mkesha   (MATTEO CIAMBELLI)

Mizinga ya maji inayonyunyizia maji baridi, iliyowekwa kando ya njia, inatoa kiburudisho cha kuburudisha kwa matembezi yao. Wakati hatimaye wataona uwanja mkubwa sana kwa hatua kubwa, ambapo Papa atasali na kuumega mkate wa Ekaristi pamoja nao, na hivyohawawezi kujizuia kutoa kilio cha kitulizo na furaha!

Maji ya kuburudisha vijana
Maji ya kuburudisha vijana   (MATTEO CIAMBELLI)

Kwenye uwanja mkubwa sana wa  Tor Vergata, mawazo yao yanaenda kasi ili kuunda njia  bora zaidi, kwa ajili yao na kundi lao. Turuba na miavuli zimefungwa kwenye vikwazo ili kutoa kivuli kikubwa iwezekanavyo. Taulo za ufukweni, miwani ya jua, na mafuta mengi ya kujikinga na jua: baadhi ya watu wamelala kwenye jua, wakipitisha muda.

Watawa wako mstari wa mbele na vijana
Watawa wako mstari wa mbele na vijana   (ANSA)

Mabango yenye majina ya majimbo  yao, jiji lao, kikundi chao cha parokia, jumuiya yao ya kiroho ni vitu vya mpito, na mablanket, ambazo zinawaweka pamoja katika nafasi hii ya ajabu na isiyo na mipaka, kati ya Tanga la Calatrava na milima ya Castelli Romani: wanasaidia vijana hawa sana, wengine labda kuwa na uzoefu wao kwa mara ya kwanza kuwa mbali na wazazi wao, ili kujisikia karibu kidogo na nyumbani.

Furaha ya vijana  katika maandalizi ya mkesha
Furaha ya vijana katika maandalizi ya mkesha   (ANSA)
Vijana Tor Vergata 2 na 3 Agosti

 

02 Agosti 2025, 14:54