MAP

2025.08.13 Kardinali Koovakad huko  Temuco nchini Chile. 2025.08.13 Kardinali Koovakad huko Temuco nchini Chile. 

Kard.Koovakad,Chile:Dini na Tamaduni katika Mazungumzo ya Amani

Mwenyekiti wa Baraza la kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini alitoa hotuba yake tarehe 13 Agosti 2025 katika mkutano wa kimataifa wa siku mbili uliofunguliwa tarehe 12 Agosti 2025 katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Temuco nchini Chile.Mada za majadiliano zilijumuisha wingi wa kidini na uhuruna mchango ya dini katika maendeleo na amani ya binadamu.Kwa njia hiyo alifafanua juu ya Vatican na mipango ya amani,diplomasia ya Vatican pia mazungumzo kupitia dini na utamaduni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali George Jacob Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Mazungumzo ya Dini Mbalimbali, alielezea mtazamo wa kiti Kitakatifu Vatican  katika kukuza amani wakati wa Kongamano la Kimataifa lililoongozwa na mada: Njia za Amani. Dini na Tamaduni katika Mazungumzo, yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Temuco, Chile kwa siku mbili ya  tarehe 12 na 13 Agosti 2025. Katika hotuba yake iliongozwa na mada ya "Kujenga amani duniani kupitia mazungumzo na ushirikiano kati ya dini, tamaduni na mataifa: Kujitolea na ushiriki Vatican.”

Utume wa Vatican wa kukuza amani 

Kardinali Koovakad alielezea juu ya  utume wa Vatican  wa kukuza amani kwa njia ya ukweli, haki, huruma, udugu, mazungumzo, upatanisho, na kazi ya kibinadamu. Aliakisi kadhali juu ya  jukumu la Papa kama Daraja kwa maana ya  kuwa mjenzi wa madaraja na akakumbusha ombi la Papa kuhusu amani lililotlewa katika hotuba ya Mtakatifu Paulo VI  kunako mwaka 1965 katika  Baraza la Umoja wa Mataifa, lakini pia hata kwa maelezo ya Papa Francisko kuhusu vita vya tatu vya dunia vilivyogawanyika  vipande vipande na wito wa Papa Leo XIV wa 2025 wa kujenga madaraja kwa njia ya mazungumzo na kukutana. Kardinali Koovakad katika hotuba hiyo alinukuu hata mipango kama vile Amani Duniani ya waraka wa “Pacem in Terris”,  Siku ya Amani ya Dunia ya kila mwaka, mkutano wa kidini wa kunako  1986 jijini  Assisi, na hati za hivi karibuni za Papa Francisko:  Laudato si’(Sifa kwa Bwana), Fratelli tutti,(Wote ni Ndugu)  na Hati ya Udugu wa Kibinadamu.

Vatican inadumisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi 184

Kwa njia hiyo Kardinali huyo alisisitiza kuwa Vatican  inadumisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi 184, Umoja wa Ulaya, na Shirika la Kijeshi ya Malta, na kwamba Vatican ina hadhi ya kudumu ya waangalizi katika Umoja wa Mataifa.  Kwa njia hiyo Kardinali Koovakad alieleza juu ya  kazi ya Vatican ya kidiplomasia inayozingatia haki za binadamu, haki ya kijamii, amani na maendeleo, mara nyingi hujihusisha na upatanishi na kuunga mkono mipango ya kimataifa kama vile Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Vatican na juhudi za mazungumzo ya kidini na kiutamaduni

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  mazungumzo ya kidini  pia alisisitiza juhudi za Vatican  katika mazungumzo ya kidini na kiutamaduni kupitia  mabaraza ya Kipapa ya Mazungumzo, La Utamaduni na Elimu na Baraza la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Juhudi hizi ni pamoja na mikutano ya pande mbili na ya kimataifa, ushirikiano na Baraza la Makanisa Ulimwenguni, na mipango ya kukuza kuheshimiana, kuelewana kiutamaduni, na kujali kazi ya uumbaji. Kardinali Koovakad alihitimisha hotuba yake  kwa kusisitiza kuwa  amani lazima ijengwe siku zote na ni wajibu wa wote, si tu serikali au taasisi za kidini. Alitoa wito wa ushirikiano wa kivitendo unaochochewa na utu wa binadamu na manufaa ya wote.

Utamaduni wa kukutana

Kardinali Koovakad akisema: “Papa Francis alisema, "utamaduni wa kukutana na utamaduni wa mazungumzo; hii ndiyo njia pekee ya amani"Pia alitetea kukuza “utamaduni wa kujali” unaojenga uhusiano wa kindugu, kukuza mshikamano na kukuza manufaa ya wote kwa ajili ya amani. Lakini amani, kama Katiba ya Kichungaji Gaudium et Spes ilivyoweka wazi, “haitapatikana mara moja kwa wote, bali lazima ijengwe daima. Ni jukumu letu sote kukuza utamaduni wa amani na kufanya kazi kuelekea amani ya ulimwengu. Na sisi, waamini na wasioamini vile vile, tuitikie mwaliko wa Papa Leo XIV wa kuleta amani “kupitia tafakari na praxis inayochochewa na hadhi ya mtu na manufaa ya wote”

13 Agosti 2025, 16:55