MAP

2025.08.20 Mkutano wa Baraza la  Maaskofu Nchini Peru. 2025.08.20 Mkutano wa Baraza la Maaskofu Nchini Peru. 

Kard.Grech kwa Maaskofu wa Peru:Kuweni Kanisa linalofungua mikono wazi na kukaribisha wote!

Katibu Mkuu wa Sinodi,Kardinali Grech aliwahimiza Maaskofu waliokusanyika katika Mkutano wao mjini Lima,nchini Peru kuendelea “kuzungumza katika Roho ambayo inachochea mazoea mapya ya kichungaji na kupendekeza miundo muhimu ya sinodi ili kukita mizizi katika jumuiya za kikanisa mahalia.”

Vatican News

Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi aliwahutubia Maaskofu wa Peru wakati wa kuadhimisha Mkutano Mkuu wa 129 wa Baraza la Maaskofu wa nchi hiyo ulioanza tarehe 18 Agosti katika mji mkuu Lima hadi 21 Agosti 2025.  Katika hotuba hiyo Kardinali alisema: "Kuzungumza katika Roho husaidia kutambua sauti hiyo inayotoka Juu, ambayo inaongoza uwongofu wa kibinafsi na wa jumuiya, inahamasisha mazoea mapya ya kichungaji, na kupendekeza miundo muhimu ya sinodi ili kukita mizizi katika Makanisa yenu mahali." Katika ujumbe wa sauti uliotangazwa tarehe 19 Agosti 2025, Kardinali huyo alisema alivyofurahishwa na kwamba maaskofu wa Peru wamechagua "kama kanuni ya dhahabu" ya mkutano wao wa njia ya sinodi ya "mazungumzo katika Roho," ambayo msingi wake ni kusikiliza na mazungumzo na "mizizi katika sala na uwazi kwa pumzi ya Roho Mtakatifu."

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la maaskofu nchini Peru
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la maaskofu nchini Peru

"Mkutano wenu unachukua tabia ya mafungo ya kweli ya kiroho, zaidi ya mkutano rahisi wa shirika. Ni wakati wa neema, ambapo Roho anazungumza na moyo wa Kanisa kupitia mioyo ya wachungaji wake," Kardinali Grech alisisitiza. Mazungumzo katika Roho, inamaanisha kujiruhusu kupingwa na mienendo ya ndani ambayo Roho huchochea ndani ya kila mmoja wenu na kati yenu, kuzingatia sio tu kwa maneno, lakini pia kwa ukimya, mawazo  na hisia za kiroho zinazojitokeza katika kubadilishana mawazo  kidugu," alisema Kardinali."

I vescovi durante la "conversazione nello Spirito"

Maaskofu wakati wa kujadiliana kiroho

Uwepo wa mazungumzo na upendo

Katibu Mkuu wa Sinodi pia alikumbusha kutiwa moyo na Papa, saa chache baada ya kuchaguliwa kwake tarehe 8 Mei  kuwa "Kanisa la kimisionari, Kanisa linalojenga madaraja na mazungumzo, daima liko wazi kwa kukaribisha (...) kwa mikono miwili kwa wote, kwa wale wote wanaohitaji upendo wetu, uwepo wetu, mazungumzo na upendo wetu.” Kwa kukaribisha kwa furaha tendo ambalo Maaskofu wa Peru wako wanajikita kwa undani juu ya Hati ya mwisho ya Sinodi(,) wakati wa mkutano wao, Kardinali Grech aliwaalika kutafakari kuhusu Muhtasari wa Awamu ya Utekelezaji wa Sinodi, (,) ambao “unaweza kutoa mfumo wa kutafakari ili matunda ya kazi yenu iweze kuchangia katika utambuzi mpana zaidi wa kikanisa.”

I partecipanti all'assemblea plenaria della Conferenza episcopale peruviana

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Peru wakishirikishana.

Hotuba ya Kardinali Mari Grech
21 Agosti 2025, 11:00