Ziara ya Kitume ya Askofu Mkuu Gallagher Nchini India: Diplomasia
Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa, kuanzia Dominika tarehe 13 hadi Jumamosi tarehe 19 Julai 2025 anafanya hija ya kitume nchini India. Lengo la ziara hii ya kitume ni kuimarisha mahusiano na mafungamano ya kidiplomasia, urafiki na ushirikiano kati ya India na Vatican.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa, kuanzia Dominika tarehe 13 hadi Jumamosi tarehe 19 Julai 2025 anafanya hija ya kitume nchini India. Lengo la ziara hii ya kitume ni kuimarisha mahusiano na mafungamano ya kidiplomasia, urafiki na ushirikiano kati ya India na Vatican.
Itakumbukwa kwamba, tarehe 12 Juni 1948 nchi hizi mbili zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na mwaka 2023, ziliadhimisha Jubilei ya Miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia. Mtakatifu Yohane Paulo II tangu tarehe 5-7 Novemba 1999 alifanya hija ya kitume nchini India.
14 Julai 2025, 14:35