ÐÓMAPµ¼º½

Mkutano wa kuwakilisha Jubilei ya vijana kutoka Ulimwenguni kote. Mkutano wa kuwakilisha Jubilei ya vijana kutoka Ulimwenguni kote.   (@Vatican Media)

Jubilei ya vijana:Roma iko tayari kuwapokea vijana Julai 28-Agosti 3!

Jubilei ya vijana,itawaona jijini Roma kwa ajili ya kipindi kilichotarajiwa sana.Katika uwakilishi kwa waandishi wa habari,ulitolewa mhutasari wa yale yatakayojiri kwa vijana ambao wataona Jubilei yao kuanza Julai 28 hadi Agosti 3 kutoka nchi 146.Askofu Mkuu Fisichella alisema:Pia ni kukumbatia kwa mawazo hasa sehemu zenye migogoro!

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia Jumatatu Julai 28 hadi Dominika tarehe 3 Agosti 2025, inaadhimisha Jubilei ya vijana ambayo inategemewa sana na ushiriki mkubwa wa tukio la Jubilei ya Mwaka Mtakatifu 2025, kwa mamia elfu ya vijana ambao wanafika Roma kutoka Nchi 146 uimwenguni waliojiandikisha.  Kwa namna ya pekee, katika mkesha wa Sala na Papa Leo XIV, kwa takriban mahujaji milioni moja wanatarajiwa Jumamosi, tarehe 2 Agosti 2025 na ambapo idadi hiyo itaongezeka pamoja na Misa Takatifu ya Dominika tarehe 3 Agosti saa 3:00 kamili asubuhi, itakayoongozwa na Baba Mtakatifu huko Tor Vergata, Roma. Kwa njia hiyo katika uwakilishi kwa vyombi vya habari Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji alieleza kwamba Jubilei ya Vijana inawakilisha "wakati unaotarajiwa zaidi" wa Mwaka Mtakatifu, "kwa sababu ndiyo iliyohudhuriwa zaidi." Mahujaji wanatoka nchi 146 tofauti, huku 68% wakitoka Ulaya, wakifuatiwa na mabara mengine. Kutajwa maalum huenda kwa vijana wanaowasili kutoka maeneo ya vita: Lebanon, Iraq, Myanmar, Ukraine, Israel, Syria, na Sudan Kusini, kwa "kukumbatia" ubora wa ambao watashirikisha vizazi vipya kutoka duniani kote.

Vijana kugawanyika katika vituo vya mapokezi

Jumatatu, tarehe 28 Julai 2025, siku hiyo itakuwa ya  kuwasili kwa mahujaji vijana katika malazi yao kwenye maeneo ya mapokezi yaliyotambuliwa jijini Roma na mkoa wa Lazio kwa ujumla na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, kwa ushirikiano na Ofisi ya Kamishna wa Serikali ya Italia, Idara ya Kitaifa ya Ulinzi wa Raia, Makao Makuu ya Wilaya na Polisi, Vicariate ya Roma, na majimbo ya mkoa wa Lazio. Takriban Parokia 370, maeneo ya shule 400, na mengine 40 ya ziada ikiwa ni pamoja na Vituo vya Ulinzi wa Raia, kumbi za michezo, na kumbi za michezo za manispaa, pamoja na familia kadhaa ambazo zimejitolea kuwakaribisha mahujaji hao vijana.

Kituo cha Maonesho cha Roma kitakaribisha vijana 25,000, ambacho kikitoa vifaa vyake ili kuhakikisha makazi salama na ya starehe. Shukrani kwa usaidizi wa uendeshaji wa Idara ya Kitaifa ya Ulinzi wa Raia, kituo hicho kitakuwa "mji ndani ya jiji" la kweli, lenye vituo vya matibabu na huduma za masaa 24. Juhudi hizi za shirika zinaonesha dhamira ya pamoja ya kutoa kwa mahujaji vijana sio tu mahali pa kulala, lakini pia uzoefu wa kweli wa jamii, na kwa usalama kamili.

Shukrani kwa serikali ya Italia

Askofu mkuu aliishukuru serikali ya Italia kwa "ushiriki wake wa kila siku" katika kuandaa hafla hizo. Kisha akatoa muhtasari wa programu ya siku hizo. Mazungumzo na Jiji yataanza tarehe 29 Julai, yakijumuisha matukio 70 yatakayofanyika katika viwanja vya Roma siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi. Mnamo tarehe 1 Agosti, "siku ya toba" itafanyika katika Uwanja wa (Circus Maximus,) na mapadre 200 wakibadilishana kila baada ya saa mbili chini ya mahema makubwa yaliyowekwa ili "kutoa ahueni" kutokana na joto kali.

Mnamo tarehe 2 Agosti 2025 milango ya Tor Vergata itafunguliwa saa 3:00 kamili asubuhi masaa ya Ulaya ambapo itakuwa  saa 4.00 kamili  masaa ya Afrika Mashariki na kati na bendi na watumbuizaji mbalimbali wataburudisha umati hadi saa 2:30 usiku, wakati mkesha na Papa Leo XIV utaanza. Kwa hafla hiyo, vijana watatu kutoka Italia, Mexico, na Marekani watamuuliza Papa maswali, na Papa "atajibu kwa lugha zao." Vile vile Askofu Mkuu Fisichella alishukuru Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa kutekeleza programu ya Vatican Vox na kwa huduma za Radio Vatican zitakazotoa tafsiri na ufafanuzi katika lugha nane. Pia kuna kitabu cha mwongozo kilichoundwa na Idara ya Ulinzi wa Raia "ambacho lazima kijulikane kwa upana iwezekanavyo na maagizo yote ya kupata wakati huu kwa utulivu kamili."

 

25 Julai 2025, 15:28