ÐÓMAPµ¼º½

Mheshimiwa Padre Richard Laurean Tiganya, wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, C.PP.S., tarehe 18 Juni 2025 ameteuliwa kuwa Gambera mpya wa Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Seregea, Jimbo kuu la Dar es Salaam Mheshimiwa Padre Richard Laurean Tiganya, wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, C.PP.S., tarehe 18 Juni 2025 ameteuliwa kuwa Gambera mpya wa Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Seregea, Jimbo kuu la Dar es Salaam 

Padre Richard Laurean Tiganya, C.PP.S., Gambera wa Seminari Kuu Mt. Karoli Lwanga, Segerea!

Itakumbukwa kwamba, Dr. Padre Richard Laurean Tiganya alizaliwa tarehe 11 Juni 1968, huko Nyakalaula, Parokia ya Ngote, Jimbo Katoliki la Bukoba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kimisionari, tarehe 19 Oktoba 2002 alipokelewa rasmi Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, Kanda ya Tanzania. Tarehe 20 Oktoba 2002 akapewa Daraja ya Ushemasi na hatimaye akapadrishwa tarehe 12 Julai 2003. Amewahi kuwa Paroko na Mhazini wa Shirika.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC., tarehe 18 Juni 2025 limemteuwa Mheshimiwa Padre Richard Laurean Tiganya, wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, C.PP.S., kuwa Gambera mpya wa Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Seregea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huu, Padre Richard Laurean Tiganya alikuwa ni Mwalimu na Mlezi, Seminari kuu ya Segerea na anachukua nafasi ya Padre Thobias Ndabhatinya ambaye amemaliza muda wake wa uongozi. Itakumbukwa kwamba, Dr. Padre Richard Laurean Tiganya alizaliwa tarehe 11 Juni 1968, huko Nyakalaula, Parokia ya Ngote, Jimbo Katoliki la Bukoba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kimisionari, tarehe 19 Oktoba 2002 alipokelewa rasmi Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, Kanda ya Tanzania. Tarehe 20 Oktoba 2002 akapewa Daraja ya Ushemasi na hatimaye akapadrishwa tarehe 12 Julai 2003.

Padre Richard Laurean Tiganya, Gambera wa Seminari kuu ya Segerea
Padre Richard Laurean Tiganya, Gambera wa Seminari kuu ya Segerea

Tangu wakati huo, alibahatika kuwa Paroko-usu Parokia ya Chibumagwa, Jimbo Katoliki la Singida, kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2004. Kati ya Mwaka 2004 hadi 2006 akateuliwa kuwa Paroko-usu Parokia ya Itigi, Jimbo Katoliki la Singida na wakati huo huo akiwa ni Padre Mhudumu wa maisha ya kiroho kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspar, Itigi, Singida inayojipambanua kwa kauli mbiu: Elimisha, Tibu na Fariji. Hatimaye kati ya Mwaka 2006 hadi mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Damu Takatifu ya Yesu, Tegeta, Jimbo kuu la Dar Es Salaam. Kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2013 alitumwa na Shirika jijini Roma ili kuongeza ujuzi na maarifa na akabahatika kujipatia Shahada ya Uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran. Kati ya Mwaka 2013 hadi mwaka 2015 alizama katika Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa na hatimaye, akahitumu kunako mwaka 2015 na kurejea nchini Tanzania.

Majando kasisi Seminari kuu
Majando kasisi Seminari kuu

Kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2019 alichaguliwa kuwa Mhasibu wa Shirika ya Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, Kanda ya Tanzania. Kati ya Mwaka 2019 hadi mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Chibumagwa, Jimbo Katoliki la Singida. Na tangu mwaka 2021 akatumwa kwenda Seminari kuu ya Mtakatifu Kaloli Lwanga, Seregea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam kuwa Mwalimu na Mlezi. Na Sasa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania imemteuwa kuwa Gambera mpya wa Seminari kuu ya Mtakatifu Kaloli Lwanga, Seregea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. Pamoja na shughuli zote hizi, lakini Padre Richard Laurean Tiganya, wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, C.PP.S., kuanzia mwaka 2021 alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Kanisa, Jimbo kuu la Dar es Salaam na Mhamasishaji wa Haki katika mchakato wa kumtangaza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa ni Mwenyeheri! Wakati wote wa masomo yake mjini Roma, alishiriki kuandaa tafakari ya Liturujia ya Neno la Mungu, Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. Dr. Richard Tiganya anafahamu lugha zifuatazo: Kihaya kama lugha Mama, Kiswahili, Kiitalia, Kiingereza na Kilatini za lugha nyingine...!

Padre Tiganya Gambera
21 Juni 2025, 14:21