ÐÓMAPµ¼º½

Padri Prof. Juvenalis Asantemungu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wa muda kuanzia tarehe 16 Juni, 2025. Padri Prof. Juvenalis Asantemungu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wa muda kuanzia tarehe 16 Juni, 2025.   (TANZANIA EPISCOPAL CONFERENCE)

Padre Juvenalis Asantemungu Ateuliwa Kukaimu Chuo Kikuu cha SAUT

Askofu Wolfgang Pisa, OFMCap., Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC kutokana na madaraka aliyo nayo kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Chuo cha SAUT ya Mwaka 2010, amemteua Padri Prof. Juvenalis Asantemungu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wa muda kuanzia tarehe 16 Juni, 2025. Uteuzi huu unafuatia changamoto ya afya anayokabiliana nayo Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu kwa wakati huu.

Na Sarah Pelaji, - Vatican

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Kansela wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT), Mhashamu Wolfgang Pisa, OFMCap., kutokana na madaraka aliyo nayo kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Chuo cha SAUT ya Mwaka 2010, amemteua Padri Prof. Juvenalis Asantemungu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wa muda kuanzia tarehe 16 Juni, 2025. Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya SAUT. Padri Prof. Asantemungu anachukua nafasi hiyo kwa muda ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu kutokana na changamoto ya afya na kutokuwepo kwa muda mrefu kwa Makamu Mkuu wa Chuo aliyepo sasa, Balozi Prof. Mahalu ambapo kulihitajika kuchukuliwa hatua maalum.

Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu
Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu   (TANZANIA EPISCOPAL CONFERENCE)

Aidha taarifa hiyo inaeleza kwamba, Makamu Mkuu wa Chuo wa muda aliyechaguliwa, Padri Asantemungu, ataendelea pia kutumikia nafasi yake kama Mkuu wa Chuo Kishiriki Cha Askofu Mkuu Mihayo cha Tabora (AMUCTA). Chuo hicho kinampongeza Prof. Asantemungu na kinamtakia mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake mapya, na kinaiomba jamii ya SAUT pamoja na umma kwa ujumla kumpa ushirikiano unaohitajika. Hadi uteuzi huo mpya wa muda, Profesa Mahalu ameongoza Chuo Kikuu cha SAUT kama Makamu Mkuu wa Chuo kwa takribani miaka saba ambapo aliteuliwa kushika nafasi hiyo mnamo Mosi, Machi 2019 na Askofu mkuu Gervas J. M. Nyaisonga akiwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Profesa Mahalu, Balozi na Mwanasheria aliyebobea alichukua nafasi ya Padre Thadeo Mkamwa, ambaye alikwenda masomoni ili kuongeza ujuzi na maarifa zaidi.

Uteuzi SAUT
17 Juni 2025, 10:43