Kardinali Parolin:maumivu na huzuni kwa Ukraine,ukosefu wa uaminifu kati yao!
Vatican News
Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin alionyesha "huzuni" na "maumivu" kwa vita vya Ukraine ambavyo vinaonekana kutokuwa na suluhisho. Kardinali, akiwa kando ya tukio huko Roma ya Tume ya Kipapa ya Akiolojia Takatifu, alisema Mimi, nafikiri kwamba tatizo la msingi ni kujenga upya hali ya kuaminiana kati ya pande hizo mbili, ambayo kimsingi inakosekana. Hatuaminiani, kwa hivyo hatuko tayari kufanya makubaliano. Na kwa hivyo la muhimu ni kwamba kuna hali hii ya hewa ambayo inaturuhusu kuzungumza moja kwa moja, kwa njia ya kujenga. Kulingana na Kardinali Parolin, inahusu "kujenga uhusiano katika hatua ndogo, yaani, kwa kusaidiana": "Ninaamini kwamba katika mazungumzo yote kuna njia ya maelewano kuchukuliwa na ni maelewano na heshima ya ahadi iliyotolewa ambayo husaidia kujenga uaminifu."
Matumaini ya amani
Kanisa, kwa upande wake, “linaweza kuombea amani,” kwa sababu “tunaona kwamba jitihada za wanadamu hazitoshi. Kama Vatican tumetoa kwa upande wetu uwezekano wa nafasi, toleo hili ambalo Papa alitoa mwanzoni mwa upapa linabaki. Lakini siamini kutokana na majibu ambayo tumepewa kwamba kuna matumaini kwamba uwezekano huu utatumiwa vibaya.”
Kuhusu hali halisi inayoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza, Kardinali Parolin alikumbuka mazungumzo yanayoendelea huko Doha, akielezea matumaini kwamba "watakuwa na matokeo fulani. Tatizo daima ni sawa: kusitishwa kwa mapigano, kurejea kwa mateka wote, walio hai na waliokufa, upatikanaji salama wa misaada ya kibinadamu na matibabu," alisisitiza.
Alipoulizwa kuhusu kugunduliwa nchini Syria kwa mwili wa mtawa mmoja katika kaburi la alaiki ambalo baadhi wameeleza kuwa ni la Padre Paolo Dall’Oglio, Kardinali Parolin alinukuu maneno ya Balozi hko Damasco, Kardinali Mario Zenari, ambaye kwa mujibu wake "hakuna uthibitisho wa ugunduzi huu. Ninaamini ni vigumu sana, tunatumaini kwamba mahali pa kuzikwa na mabaki ya Padre Dall'Oglio yanaweza kupatikana. Baada ya miaka mingi hivyo, ni vigumu kumfikiria akiwa hai,”alisema
Mkutano wa Papa na Sekretarieti ya Vatican
Alipoulizwa kuhusu Mkutano wa Papa Leo XIV na Sekretarieti ya Vatican, ulipangwa tarehe Juni 5, Kardinali Parolin alikumbuka kwamba itakuwa mkutano wa kwanza rasmi na Papa lakini kwamba "ushirikiano tayari umeanza tangu wakati wa kwanza wa papa. Ninaamini kwamba atatumia chombo hiki alicho nacho kwa usahihi kwa ajili ya uongozi wa Kanisa.” Kardinali huyo alisisitiza kuwa “Papa alisema tangu mwanzo kwamba anakusudia kutumia kwa njia ya pamoja vyombo vyote vilivyo mikononi mwake ili kuhakikisha uongozi mzuri wa Kanisa.”