MAP

2025.06.19 Wakati wa Jukwaa la kidini kwa ajili ya amani katika nchi za Balkani. 2025.06.19 Wakati wa Jukwaa la kidini kwa ajili ya amani katika nchi za Balkani. 

Jukwaa la mazungumzo na amani katika Balkan,warsha la vijana mafundi wa amani!

Gleison De Paula Souza,katibu wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha,alishiriki katika Jukwaa la kidini lililoandaliwa huko Koper na Baraza la Maaskofu wa Slovenia:maadili ya kibinadamu lazima yatetewe ili kukuza amani na ubunifu wa "volkano" ya vizazi vichanga lazima uthaminiwe.

Vatican News

"Vijana wameitwa kwa kazi ya ujasiri: kujenga urafiki wa kijamii, kuondokana na migawanyiko ya kihistoria na kiutamaduni na kuwa 'mafundi wa amani'. Na hatua ya kwanza ya kuwa watendaji wa amani ni kuchagua mazungumzo. Huu ni uchaguzi unaohitaji kusikiliza na mara nyingi kushinda majeraha ya kihistoria. " Hayo yalisemwa na Gleison De Paula Souza, katibu wa Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha, akizungumza Jumamosi tarehe 14 Juni 2025 huko Koper, Slovenia, kwenye "Jukwaa la Mazungumzo na Amani katika Balkan 2025 - Maadili ya Pamoja ya Maisha kwa Amani."

Mkutano huo wa kidini uliandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Kislovenia, nyeti kwa ufuatiliaji wa matokeo ambayo inaonesha kurudi kwa vita tena  Ulaya Mashariki, na mzozo kati ya Urusi na Ukraine, kunaweza kusababisha katika muundo wa kijamii wa idadi ya watu wa Balkan: kufungua tena majeraha ya zamani ya kumbukumbu, baada ya mapigano ya umwagaji damu kati ya makabila ambayo yaliharibu Yugoslavia ya zamani katika miaka ya 1990.

Jukwaa la mazungumzo na amani huko Balkan
Jukwaa la mazungumzo na amani huko Balkan

Balkan, maabara ya amani

Kwa sababu hiyo  na vile vile kwa ajili ya umuhimu wake wa kijiografia katika bara la Ulaya na utata wa ajabu wa kikabila, lugha na kidini", mwakilishi wa Vatican  alisisitiza uwezo wa ajabu wa eneo la Balkan kama "maabara hai ambapo kuthaminiwa kwa utofauti kunawakilisha changamoto kubwa na utajiri mkubwa".

Vijana na maadili

"Maadili ya maisha, kama vile upendo, haki, mshikamano, utu - alisema katibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kuwa  - inahitaji amani ili kukuza, lakini kinyume chake pia ni kweli: hakuwezi kuwa na amani ikiwa hatutetei maadili ambayo yanalinda maisha." Kwa usahihi katika utetezi huu wa maadili, De Paula Souza aliona kazi ya upendeleo ya vijana: "Wao ni volcano ya maisha, ya nguvu, ya hisia, ya mawazo  na kwamba  wana uhai na uimara, mfano wa umri mdogo, ambao ni sifa za kuchochea na kuzaa ambazo zinaweza kuunda mwanga na ustaarabu wa kibinadamu zaidi".

Uhai wa vijana unaweza kubadilisha ulimwengu

Kwa hivyo jukumu la siasa na taasisi kuwezesha kujieleza huru kwa uwezo wa vizazi vipya na wakati huo huo kuweza kuelewa mahitaji ya mabadiliko: "Mwaliko wake kama waendeshaji wa kisiasa, kiutamaduni, kidini na kijamii, ni kuwakaribisha na kusindikizana  na vijana na kuwaacha vijana wenyewe waambatane nasi na kuamsha dhoruba yetu kwa nguvu hiyo ya uzalishaji ambayo inafanya dunia kubadilika,” alihitimisha De Paula Souza -

19 Juni 2025, 12:56