ĐÓMAPµĽş˝

Jubilei ya harakati na vyama:"Sisi ni matawi tofauti ya mti mmoja"

Sauti na ushuhuda wa baadhi ya waamini elfu 70 kutoka duniani kote katika hija ya kupita katika Milango Mitakatifu ya Makanisa Makuu ya Kipapa kwa ajili ya tukio linalohusisha harakati za kikanisa.Mkutano na Papa Leo XIV katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,jioni Juni 7 kwa ajili ya Mkesha wa Pentekoste na Juni 8 kuadhimisha misa ya kuhitimisha Jubilei yao.

Vatican News

"Matawi ya mti yana kila aina ya maumbo na saizi, na huchukua mwelekeo tofauti kutoka kwa kila mmoja, lakini kila wakati hutafuta mwanga." Hivi ndivyo Emilia González kutoka Panama, wa Cursillos de Cristiandad, alijaribu kueleza ukweli wa mchanganyiko wa mikusanyiko ya kikanisa ambayo tangu asubuhi ya  Jumamosi tarehe 7 Juni 2025 wamekuwa wakivuka Milango Mitakatifu ya Makanisa Makuu mbalimbali ya kipapa katika maadhimisho ya Jubilei ya harakati, vyama na jumuiya mpya.

Hija ya Jubilei
Hija ya Jubilei

Cheche mpya

"Kila mmoja wetu, kwa njia yake mwenyewe, anataka kuleta lishe kwa Kanisa kupitia utajiri wetu wa kiroho na wa kimisionari kwa njia tofauti za kumfuata Yesu.

Hii ni zawadi kubwa ya ushirika na ushuhuda wa kujitolea kwa mafundisho ya Baba Mtakatifu”, aliongeza mwanamke huyo aliyefika Roma akiwa na wenzao wapatao arobaini kutoka katika Harakati  iliyozaliwa mwaka 1944.

Hija ya Jubilei
Hija ya Jubilei

Akitoka katika nchi iliyoandaa Siku ya Vijana Duniani kwa mwaka wa 2019, Emilia alisisitiza kwa vyombo vya habari vya Vatican jinsi "kusanyiko hili la jumla" na Papa Leo XIV pia ni "chemchemi kubwa ya matumaini na cheche mpya ya kuishi Ukristo kwa kugundua upendo wa Mungu, huruma ya Yesu na mwanga wa Roho Mtakatifu".

Kumbe, majumuisho ya Makanisa yatashiriki mkesha wa Pentekoste kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro usiku wa kuamkia tarehe 8 pamoja na Askofu wa Jimbo kuu la Roma,yaani Papa Leo XIV ambaye Dominika  ataadhimisha misa takatifu kwa ajili yao katika ukumbi wa Kanisa kuu la Vatican.

Kwa sababu hiyo, tayari saa za asubuhi na mapema, Uwanja wa  Pia uliko mbele ya Jengo la Radi Vatican, ulijaa waamini kutoka kila kona ya dunia, wenye shauku ya kukamilisha sehemu ya mwisho ya barabara kuelekea Mlango Mtakatifu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, wakiwa wamebeba msalaba wa matumaini.

"Mama" wa Congo

Kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakiwa wamevalia nguo za kiutamaduni za rangi za rangi, alikuwa ni Françoise na Madeleine: wa Umoja wa Mama wakatoliki na ni wa harakati iliyoanzishwa Kinshasa mwaka 1986 na Kadinali Joseph-Albert Malula kuleta pamoja wanawake walioolewa au wasio na watoto, walio na au wasio na watoto, kulingana na "wito wa umama katika Kanisa" juu ya mfano wa Maria. Madeleine, umri wa miaka 70, kwa miaka thelathini alitumia muda wake akiwa ndani ya umoja huo ulioenea katika nchi ya Afrika, ambaye alizungumzia juu ya jukumu la "mama", ambao wanasaidiana na kusindikiza  jumuiya za kikanisa, wakati Françoise alikubali, akisubiri kuvuka Mlango Mtakatifu,alihisi "kutetemeka kidogo" kwa hisia kali.

 

07 Juni 2025, 18:03