MAP

2025.06.18 Kardinali Grech akiwa na Patriaki wa Costantinopoli, Bartolomeo I. 2025.06.18 Kardinali Grech akiwa na Patriaki wa Costantinopoli, Bartolomeo I. 

Kard.Grech huko Istanbul,akutana na Bartholomew:tunaunda madaraja katika enzi ya mgawanyiko

Katibu mkuu wa Sinodi yuko Uturuki kuwasilisha awamu ya utekelezaji wa Sinodi katika muktadha wa mkutano wa makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE).Akiwa Fanar alitoa salamu kwa Patriki wa Constantinopoli ambaye alihutubia washiriki akihimiza mazungumzo katika wakati uliowekwa na migawanyiko,hofu na vurugu.Kwa maneno ya Patriaki pia alimkumbuka Hayati Papa Francisko na matarajio ya ziara ya Papa Leo XIV katika fursa ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Ulikuwa Mkutano wa kidugu, ulioadhimishwa kwa kukumbatiana unaowakumbuka wengi waliobadilishana na Hayati Baba Mtakatifu Francisko, ambao ulifanyika alasiri ya tarehe 17 Juni 2025  kwenye Uwanja wa Fanari kati ya Patriaki wa Constantinople, Bartholomew I, na Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi, ambaye yuko  mjini Istanbul Uturuki kwa ajili ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Baraza la Maaskofu wa Ulaya (CCEE). Kardinali Grech aliwasilisha kwa washiriki wote mchakato wa kusindikiza awamu ya utekelezaji wa Sinodi. Mpango wake pia ulijumuisha kusimama huko Nicea, ambayo sasa ni Iznik, kiti cha Baraza la Kiekumene la kwanza, ambalo linaadhimisha miaka 1700 na ambapo - kama inavyojulikana inatarajiwa kufanyika  ziara ya Papa Leo XIV katika mwendelezo wa shauku ya  mtangulizi wake Papa Francisko.

Shukrani kwa Papa Francisko na furaha kwa Papa  Leo

Ilikuwa hasa kutoka katika  kumbukumbu ya Papa Francisko na "wasiwasi mkubwa" wa ziara ya Papa Leo kwamba  Patriaki Bartholomew alizungumza katika hotuba yake kwa washiriki wa  mkutano wa CCEE. Kwanza kabisa, Patriaki huyo alionesha shukrani “kwa ajili ya urafiki wa kibinafsi na dhamira isiyoyumbayumba ya Papa Francisko” (“rafiki wa kweli wa Kanisa la Kiothodox,” alimwita) ambaye upapa wake ulikuwa wakati wa uchangamfu na kutiana moyo.” Kisha alisisitiza furaha yake katika uchaguzi wa mrithi wake Robert Francis Prevost, ambaye tayari amekutana naye mara mbili. "Tuna uhakika, kwamba chini ya uongozi wake mahusiano kati ya Makanisa yetu mawili yataendelea kuwa ya kina katika ukweli na upendo. Tunasali kwamba upapa wake utambuliwe na utambuzi wa kiroho na ujasiri wa kinabii, Kanisa likiendelea kutoa ushuhuda katika ulimwengu unaotamani sana mwelekeo na umoja,”alisema Patriaki huyo

Umuhimu wa mazungumzo

Patriaki wa Konstantinopoli alijitolea nafasi ya kutosha kwa umuhimu wa mazungumzo, kiekumene na kidini, hasa katika zama hii yenye migawanyiko, hofu na vurugu" ambapo "tumeitwa kujenga madaraja, si kuta. Hasa, uhusiano na Kanisa Katoliki la Roma, mazungumzo ya kitaalimungu yalianza tena karibu nusu karne iliyopita, baada ya kufutwa kwa laana za pande zote mnamo 1965, ni msingi wa kuendelea na njia ya kukutana mara kwa mara na mbaya. Njia hakika isiyo  kosa changamoto, lakini wakati huo huo iliyoangaziwa na nyakati za neema, kwa uelewa wa ndani zaidi na hamu ya kweli ya umoja unaotamaniwa na Kristo." Kisha kuna mazungumzo na Makanisa mengine ya kale ya Mashariki, pamoja na mapokeo ya Kiprotestanti na mashirika mengi kati ya Wakristo: si "michakato rasmi", lakini "makutano ya kiroho", matukio ya "kujitolea upya kwa Injili". Na kama Kanisa la kiorthodox, "tunatilia maanani sana mazungumzo baina ya dini," alisema Mkuu wa Kiorthodox, akieleza kwamba uhusiano na viongozi wa Kiyahudi, Waislamu na viongozi wengine wa kidini umedumishwa kwa muda mrefu, kwa imani kwamba "amani, maelewano na heshima kwa utu wa kila mwanadamu lazima  viwe  ahadi za msingi kwa tamaduni  zote za kidini."

Changamoto kwa Kanisa na Binadamu

"Kiukweli, hatuko vipofu kwa changamoto nyingi ambazo Kanisa na ubinadamu wanakabiliana nazo leo. Masuala ya haki ya kijamii, uhamiaji, vita, mateso ya kidini na mgogoro wa hali ya hewa yanahitaji umakini wetu. Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kutenganishwa na Injili tunayotangaza. Utunzaji wa uumbaji, hasa, unasalia kuwa eneo ambalo ushirikiano wetu na Makanisa na taasisi nyingine umezaa matunda mengi,” Patriaki Bartholomew alisema.

Huduma ya Mabaraza ya Maaskofu ya Ulaya

Katika hali hiyo,  Patriaki  Bartholomayo alisifu na kuhimiza huduma ya Mabaraza ya Maaskofu ya Ulaya ambayo husaidia “kueleza ushuhuda wa Kanisa na kuratibu mwitikio wake kwa mahitaji ya watu.” "Unawezesha uwiano, uwazi na upendo ambao Kanisa linazungumza nao leo. Kwa kawaida, pia kulikuwa na kumbukumbu ya maadhimisho ya mwaka wa 1700 wa Baraza la Ekumeni la Nicea, ambayo "inatukumbusha kwamba umoja si suala la urahisi au mkakati, lakini uaminifu kwa ukweli uliofunuliwa katika Kristo na kutangazwa kwa njia ya maisha ya Kanisa,"alisema.

Misa iliyoadhimishwa na Kardinali Grech

Tukio hili la maridhiano pia lilikuwa kitovu cha mahubiri ya Misa Takatifu ambayo Kardinali Grech aliadhimisha katika Kanisa la Mtakatifu Anthony mjini Istanbul. Katika mahubiri yake alisema: “Tumeunganishwa mahali hapa ambapo, miaka 1700 iliyopita, Kanisa lilitangaza kwa dhati kwamba Mwana ni wa asili ileile ya Baba. Wakati huo, kwa wengi lilikuwa chaguo la kuchukiza la maneno na tusi kwa asili ya Mungu, lakini badala yake linaonesha ukuu na ujasiri wa kitaalimungu, wa wale waliohudhuria kwenye Baraza, ambao walidumisha kwamba asili ya Mungu, ingawa ni mmoja, ni shirikishi. Mwana anashiriki katika asili ya Baba. Yesu anatuita sisi watoto wa Mungu, na mtoto anashiriki katika asili sawa na mzazi,” Kardinali  Grech alisema. “Kwa upande wetu sisi wanadamu, Mungu huchukua hatua na kutupa ushiriki katika asili yake, anatuchukua. Na kwa mtazamo wetu, tunaweza kushiriki katika asili ya Mungu kwa kuiga, kutenda na kuishi kama Baba, kuwa kama Baba”.

Kuishi ushirika kwa njia ya sinodi

“Kumwiga Mungu kunamaanisha kuingia katika ushirika na wengine, kujenga madaraja ya ushirika kati ya watu mbalimbali, hata iwe vigumu vipi”, alisema Katibu Mkuu wa Sinodi, ambaye alinukuu kifungu cha Hati ya Mwisho ya Sinodi ya Maaskofu, kwa usahihi aya ya 154 inayosomeka: “Tukiishi mchakato wa sinodi, tumeongeza ufahamu kwamba wokovu unaopaswa kupokewa na kutangazwa una uhusiano wa ndani..... Roho ameweka shauku ya mahusiano ya kweli na vifungo vya kweli ndani ya moyo wa kila mwanadamu..... Tunaweza kuishi ushirika unaookoa kwa kutembea katika njia ya sinodi, katika mwingiliano wa miito yetu, karama zetu na huduma zetu, kwenda nje kukutana na kila mtu kuleta furaha ya Injili”. Hakika, kujenga madaraja ya ushirika si rahisi kamwe. Nicea na mivutano iliyotokana nayo ni mfano mzuri, kama ilivyo Sinodi ya mwisho kuhusu sinodi na mivutano na mabishano yanayohusiana. Lakini ni lazima tukumbuke kwamba sisi ni viumbe wenye ukomo, tukijaribu kuiga kile kisicho na kikomo, asili ya Mungu,” alihitimisha.

 

19 Juni 2025, 12:44