Wito wa makardinali:kujenga amani ya haki na ya kudumu bila kusita!
Vatican News
Katika mkesha wa kuanza kwa Mkutano Mkuu wa uchaguzi, tarehe 6 Mei 2025, Makardinali waliokusanyika mjini Vatican kwa ajili ya kumchagua Papa mpya, walihimiza kusitishwa kwa mapigano katika maeneo ambayo migogoro inaendelea. Wakiwa wamekusanyika katika Mkutano Mkuu, Makardinali, walibainisha kwa masikitiko kwamba 窶徂akuna maendeleo yoyote ambayo yanapatikana katika kukuza michakato ya amani nchini Ukraine, Mashariki ya Kati na sehemu nyingi za dunia窶 na kwa hiyo, wanaelezea 窶忤asiwasi wao kwa mashambulizi ambayo yamezidi hasa dhidi ya raia."
Dunia inatamani amani
Makardinali hao walisisitiza kuwa: "Tunatoa wito wa dhati kwa pande zote zinazohusika kufikia usitishaji wa kudumu wa mapigano haraka iwezekanavyo na kujadiliana, bila masharti na ucheleweshaji zaidi, amani inayotamaniwa kwa muda mrefu na watu wanaohusika na ulimwengu mzima. Mwaliko kutoka kwa Makadinali unaelekezwa kwa waamini wote kuzidisha dua kwa Mola kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu" Ndivyo tunasoma taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya ya mjini Vatican.