Utafiti wa Saratani,Huduma ya Afya na Kinga ili Kupunguza Ukosefu wa Usawa!
Vatican News
Saratani inaendelea kuongezeka kama janga la kiafya la kimataifa na visa vipya vya milioni 20 na vifo vya milioni 10 kila mwaka. Wanasayansi wakuu katika uwanja wa utafiti wa saratani, pamoja na watunga sera za afya na wawakilishi wa mashirika ya wagonjwa, walikusanyika huko Casina Pio IV, ambayo ni makao makuu ya Chuo cha Kipapa cha Sayansi, kwa siku mbili tarehe 22 na 23 Mei 2025 ili kushughulikia shida ya afya ya saratani katika sayansi na hatua mpya. Washiriki hawa wanatoka Ulaya, Afrika, Asia na Amerika.
Ingawa kuna utambuzi wa maendeleo makubwa ya kisayansi, usambazaji wake unasalia kutofautiana sana-kati ya kaskazini na kusini duniani kote, na ndani ya mataifa na maeneo binafsi. kwa njia hiyo Mkutano huo uliainisha mikakati ya kurekebisha utafiti na utunzaji wa saratani ili kupunguza ukosefu wa usawa na kujumuisha masikini. Licha ya maendeleo makubwa katika biolojia ya saratani, tofauti kubwa zinaendelea ndani ya nchi zote, zikiendeshwa na vizuizi vya kimfumo na kijamii na kiuchumi.
Mwendelezo jumuishi
Profesa von Braun, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi alisisitiza kwamba: “kuna haja ya kuwa na mwendelezo jumuishi wa utafiti wa kuunganisha sayansi ya kimsingi, matumizi ya kimatibabu, na matokeo halisi ya ulimwengu ili kuhakikisha wagonjwa wote wananufaika na maendeleo ya kisayansi.†Vipaumbele muhimu ni pamoja na kupanua Dawa ya Kutabiri, Kuzuia, Kubinafsisha, na Shirikishi ya Saratani; kuimarisha Vituo Kabambe vya Saratani (CCCs); kushughulikia afya ya kidijitali na fursa za Akili Nunde(AI;) na kupachika uchumi wa afya na sayansi ya utekelezaji.
Kuelekeza utafiti unaoofadhiliwa na umma
Mabadiliko kuelekea utafiti unaofadhiliwa na umma, unaoendeshwa na misheni ilipendekezwa kwa nguvu ili kukabiliana na utawala wa kibiashara na kuoanisha uvumbuzi wa saratani na malengo ya usawa. Umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa na uimarishaji, sio kupunguza uwezo wa mipango ya afya ya kimataifa, unaohitajika. Kwa kuwekeza katika kuzuia, ubora wa maisha na ufikiaji sawa, ajenda ya kimataifa ya utafiti wa saratani inaweza kuwa kielelezo cha mshikamano, uendelevu, na uwajibikaji wa kimaadili. Jumuiya za kidini, hasa, zinaweza kuchukua jukumu muhimu katika mazungumzo ya maadili, kutoa sauti kwa masikini na kutengwa, na kukuza mifumo ya maadili ya vitendo.