Papa anavyochaguliwa
“Eligo in Summum Pontificem”.
Makardinali 133 Wateule walioitwa kuchagua Papa wa 267 wa Roma watakuwa na mikononi mwao na karatasi ya kura ya mstatili yenye maandishi haya kwenye nusu ya juu na "mahali pa kuandika jina la wateule" kwenye nusu ya chini na "kufanywa kwa namna ambayo inaweza kukunjwa vipande viwili." Yote yameelezewa kwa kina katika Katiba ya Kitume ya .
Usambazaji wa karatasi za kupiga kura
Mara baada ya kura kutayarishwa na kusambazwa (angalau mbili au tatu kwa kila mteule mkuu) na wasimamizi wa tukio hilo, shemasi wa mwisho ambaye ni Kardinali huchota kwa kura, kutoka miongoni mwa makardinali wapiga kura wote, wakaguzi watatu, watu watatu wenye mamlaka ya kukusanya kura za Makardinali wengine (infirmarii) yaani wahudumu wa wagonjwa na waangalizi watatu. Ikiwa katika maandishi ya majina ya makardinali wapiga kura yanatoka ambao, kwa sababu ya udhaifu au sababu nyingine, hawawezi kutekeleza majukumu haya, majina ya makardinali wengine yanatolewa mahali pao. Hii ni awamu ya kabla ya uchunguzi. Kabla ya wapiga kura kuanza kuandika, katibu wa Baraza la Makardinali, Msimamizi wa Maadhimisho ya Liturujia ya Kipapa na wasimamizi wa sherehe, wanapaswa kuondoka katika Kikanisa cha Sistine, kisha shemasi wa mwisho yaani Kardinali anafunga mlango, na kufungua mara nyingi iwezekanavyo, ikiwa kutakuwa na wagongwa na aliyechaguliwa atakwenda kwa wagonjwa hao kukusanya kura za wagonjwa na kurudi kwenye Kikanisa hicho.
"Chumba cha machozi" na ambacho ndicho cha kuvaa nguo za Papa mpya)
Kura
Kila Kardinali, mteule kwa mpangilio wa utangulizi, baada ya kuandika na kukunja kura, akiishikilia ili ionekane; huipeleka kwenye madhabahu, ambapo wachunguzi husimama na juu yake na kuna chombo kilichofunikwa na sahani ili kukusanya kura." “Namwita Kristo Bwana, atakayenihukumu, ashuhudie kwamba kura yangu imetolewa kwa yule ambaye, kulingana na Mungu, naamini anafaa kuchaguliwa.”
Hayo ndiyo maneno ambayo kila Kardinali atasema kwa sauti, akiweka kura yake kwenye sahani na kuiingiza kwenye chombo. Mwishoni anasujudu madhabahu na kurudi mahali pake. Makardiali wateule walioko katika kikanisa cha Sistine ambao hawawezi kwenda madhabahuni kwa sababu ni wagonjwa, wana usaidizi wa wachunguzi wa mwisho anayewakaribia: baada ya kutamka kiapo wanakabidhi kura iliyokunjwa kwa mchunguzi ambaye anaibeba inayoonekana wazi madhabahuni na, bila kutamka kiapo hicho, anaiweka kwenye sahani na huku akiiingiza kwenye chombo.
Kikanisa cha Sistina, mahali ambapo uchaguzi wa Papa mpya utafanyika
Jinsi gani makardinali wagonjwa wanapiga kura
Ikiwa kuna makardinali wateule wagonjwa katika vyumba vyao, makardinali watatu wanaosaidia wagonjwa waitwao infirmarii wanakwenda pale wakiwa na idadi inayofaa ya karatasi ya kupiga kura kwenye trei ndogo na sanduku lililotolewa na wachunguzi na kufunguliwa hadharani nao, kwa namna ya kwamba wapiga kura wengine waone kwamba ni tupu, kisha hufungwa kwa ufunguo uliowekwa juu ya madhabahu. Sanduku hili lina shimo katika sehemu ya juu ambayo kura iliyokunjwa inaweza kuingizwa. Wagonjwa wanapiga kura kwa njia sawa na makadinali wengine, kisha wahudumu wao (infirmarii) wanarudisha sanduku kwenye Kikanisa cha Sistine, ambapo hufunguliwa na wachunguzi baada ya makardinali waliopo kuweka kura yao. Wachunguzi huhesabu kura zilizopatikana hapo na, baada ya kuhakikisha kwamba idadi yao inalingana na ile ya wagonjwa, huziweka moja baada ya nyingine kwenye sahani na kwa hili kuziingiza zote pamoja kwenye chombo.
Kuhesabu kura
Baada ya wapiga kura wote Makardinali kuweka kura zao kwenye kisandukui, mchunguzi wa kwanza anatikisa kisanduku mara kadhaa ili kuchanganya kura na, mara baada ya hapo, mchunguzi wa mwisho anaendelea kuhesabu kura kwa kuzichukua zikionekana moja baada ya nyingine kutoka kwenye chungu na kuziweka kwenye chombo kingine kitupu.Ikiwa idadi ya kura hailingani na idadi ya wapiga kura, lazima zote zichomwe na kura ya pili lazima ifanyike mara moja. Ikiwa, hata hivyo, inalingana na idadi ya wapiga kura, hufuata kuhesabu tena. Wachunguzi watatu walioketi kwenye meza iliyowekwa mbele ya madhabahu: wa kwanza huchukua kura, kuifungua, anaandika jina la mtu aliyechaguliwa na kuipitisha kwa wa pili ambaye, baada ya kujua jina la mtu aliyechaguliwa, huipitisha kwa wa tatu, ambaye anaisoma kwa sauti - ili wapiga kura wote waliopo waweke alama ya kura zao kwenye karatasi maalum - na kuandika jina lililosomwa. Iwapo, wakati wa kuhesabu kura, wachunguzi wataona kura mbili zimekunjwa ili zionekane kuwa zimejazwa na mpiga kura mmoja, ikiwa zina jina moja zitahesabiwa kuwa kura moja; ikiwa, hata hivyo, wana majina mawili tofauti, hakuna kura kati ya hizo mbili zitakuwa halali; lakini kwa vyovyote vile kura haitabatilishwa.
Baada ya kura kuhesabiwa, wachunguzi huongeza kura zilizopatikana kwa majina mbalimbali na kuziandika kwenye karatasi tofauti. Wachunguzi wa mwisho, wanaposoma kura, wanazichoma kwa sindano mahali ambapo neno Eligo linapatikana, na kuziingiza kwenye uzi, ili zihifadhiwe kwa usalama zaidi. Mwishoni mwa usomaji wa majina, ncha za uzi zinafungwa na fundo, na kura zinawekwa kwenye chombo au kando ya meza. Katika hatua hii kura zinaendelea kuhesabiwa, basi, baada ya ukaguzi wao, kura zinachomwa kwenye jiko la chuma lililotumiwa kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kunako mwaka 1939. Jiko la pili, au Chemney tangu 2005, lililounganishwa, hutumiwa kuweka aina ya kemikali ambazo lazima zitoe rangi nyeusi katika muktadha wa kutochaguliwa na rangi nyeupe katika muktadha wa uchaguzi.
Majiko mawili ambayo kadi za kupigia kura huwekwa ili kuchwa na kutoa rangi nyeusi au nyeupe (ANSA)
Idadi inayohitajika
Kwa uchaguzi wa Papa wa Roma, angalau 2/3 ya kura zinahitajika. Katika muktadha maalum wa Mkutano Mkuu utakaoanza Jumatano tarehe 7 Mei 2025, kura 89 zitahitajika kumchagua Papa, kwa kuwa idadi ya Makardinali wapiga kura ni 133. Kwa hiyo iwe Papa amechaguliwa au la, wakaguzi lazima waendelee kukagua kura na maelezo yaliyotolewa na wakaguzi, ili kuhakikisha kwamba wametekeleza kazi yao kikamilifu na kwa uaminifu. Mara baada ya mapitio hayo, kabla ya wapiga Makardinali wapiga kura kuondoka kwenye Kikanisa cha Sistine, kura zote zinachomwa moto na wachunguzi, wakisaidiwa na katibu wa Baraza la Makardinali na wasimamizi wa sherehe, zilizoitishwa wakati huo huo na Kardinali shemasi. Ikiwa, hata hivyo, kura ya pili lazima ifanyike mara moja, kura kutoka katika kura ya kwanza zitachomwa tu mwishoni, pamoja na zile za kura ya pili.
Kufungwa kwa jiko na bomba katika Kikanisa cha Sistine (ANSA)
Kupiga kura
Upigaji kura unafanywa kila siku, saa mbili asubuhi na saa 8 alasiri, na ikiwa Makardinali wapiga kura wana shida kukubaliana juu ya mtu atakayechaguliwa, baada ya siku tatu bila matokeo, kura zitasimamishwa kwa muda wa siku moja, kwa sala, mazungumzo yao kati ya wapiga kura na mafungo mafupi ya kiroho, yatakayotolewa na Kardinali wa kwanza wa utaratibu wa mashemasi. Kisha upigaji kura utaaanza tena. Baada ya kura saba, ikiwa uchaguzi hautafanyika, kupumzika tena kwa sala mazungumzo na ushauri utatolewa na Kardinali kwanza wa utaratibu wa Mapadre Kisha mfululizo mwingine unaowezekana wa kura saba unafanywa, na ikiwa matokeo hayatafikiwa, naoumziko mapaya na sala, mazungumzo na mawaidha yanaatazamiwa, kutolea na Kardinali wa kwanza wa utaratibu wa maaskofu. Kisha upigaji kura utaanza tena, zaidi ya saba. Ikiwa hakuna uchaguzi, siku imetengwa kwa sala, tafakari na mazungumzo na katika kura zinazofuata, uchaguzi lazima ufanywe kati ya majina mawili ambayo katika kura ya awali yalipata idadi kubwa zaidi ya kura. Katika kura hizo pia, wingi angalau theluthi mbili ya kura za makadinali waliopo na wanaopiga kura inahitajika, lakini katika kura hizi, makardinali wawili ambao kura zilikuwa nyingi hawawezi kupiga kura.