MAP

“Sura za Injili,”Papa Francisko asimulia tajiri na maskini

Vatican News

Kipindi cha kumi na sita kati ya 18 kinachounda "Volti dei Vangeli," yaani Sura za Injili, kilichopendekezwa tena na Vatican News katika kipindi hiki cha Pasaka, kinaakisi sura ya tajiri, asiyejali masikini mwombaji anayesimama mlangoni pake. "Watu wawili, mmoja aliridhika na maisha yake, na mwingine jina lake Lazaro ambaye aliomba sadaka. Katika Injili, kutojali kwa tajiri kunasababisha kupoteza jina lake, ni lile la maskini tu ndilo linalojulikana, tajiri ana sifa za sifa.”

Hivi ndivyo Baba Mtakatifu Francisko anavyosimulia baadhi ya matukio ya Yesu katika kipindi, kilichotangazwa katika kipindi cha kwanza kabisa Dominika ya Pasaka 2022 kwenye Runinga ia Italia (Rai Uno,) kinachosimamiwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na (Rai Cultura) Kipindi cha Radio cha Utamaduni Italia. Waandishi wa mfululizo huo ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, mwelekeo na upigaji picha uliratibiwa na Renato Cerisola, muziki asili na Michelangelo Palmacci.

28 Mei 2025, 10:46