MAP

Uharibifu wa Ukanda Gaza Uharibifu wa Ukanda Gaza  (MAJDY JILDAH)

Parolin:inatosha mabomu huko Gaza,tuombe suluhisho nchini Ukraine

Mahojiano na Katibu wa Vatican:"Sheria ya kibinadamu lazima itumike kila wakati,hali katika Ukanda huo haikubaliki.Hamas lazima iwaachilie mateka wote.Hapana kwa chuki dhidi ya Wayahudi."Na juu ya uwezekano wa mkutano wa kilele Vatican:Tumetoa upatikanaji wetu,lakini jambo muhimu sio mahali ambapo mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yatafanyika,cha muhimu ni kwamba wanaweza kuanza."

Andrea Tornielli

Picha za kutisha zinazotoka huko Gaza, shambulio la chuki dhidi ya Wayahudi huko Washington, uwezekano wa mkutano wa kilele cha amani juu ya Ukraine na mwanzo wa upapa wa Papa Leo XIV alikuwa ni miongoni mwa masuala ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, katika mazungumzo na vyombo vya habari vya Vatican akiingilia kati masuala yaliyo katikati ya umakini wa sasa wa Vatican

Mwadhama, huko Gaza watoto wanakufa kwa njaa na idadi ya watu imechoka, mabomu yanaanguka kwenye shule na hospitali. Na bado haionekani kama kuna nia yoyote ya kukomesha milipuko ...

Kinachotokea Gaza hakikubaliki. Sheria ya kimataifa ya kibinadamu lazima itumike kila wakati, na kwa kila mtu. Tunaomba kwamba milipuko ya mabomu ikome na kwamba msaada unaohitajika ufikie idadi ya watu: Ninaamini kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kila linalowezekana kukomesha janga hili. Wakati huo huo, tunasisitiza kwa nguvu wito wetu kwa Hamas kuwaachilia mara moja mateka wote ambao bado wanawashikilia, na kurejesha miili ya waliouawa baada ya shambulio la kinyama la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli.

Ulichukuliaje shambulio la hivi majuzi huko Washington, na mauaji ya wafanyakazi wawili wa Ubalozi wa Israeli?

Ilinishtua sana, kwani tayari ilitokea Oktoba 7, wao ni waathirika wasio na hatia, na hawa pia walijitolea kwa ajili ya amani na mipango ya kibinadamu. Ni lazima tuwe waangalifu na kuhakikisha kwamba saratani ya chuki dhidi ya Wayahudi, ambayo haijashindwa kabisa, hainyanyui kichwa chake tena.

Katika siku za hivi karibuni, baada ya matokeo mabaya ya mkutano huko Istanbul, kulikuwa na mazungumzo juu ya uwezekano wa mazungumzo mapya kuandaliwa mjini Vatican, hata kama upande wa Urusi ulisema "hapana." Unaweza kutuambia nini kinaendelea katika suala hili?

Papa Leo alitoa uwezekano wake kamili wa Vatican kuandaa mazungumzo yoyote, kwa kutoa nafasi ya kutoegemea upande wowote, mahali penye ulinzi. Kwa hiyo haikuwa upatanisho, kwa sababu upatanisho lazima uombwe na wahusika. Katika muktadha huo,  hata hivyo, kulikuwa na toleo la umma tu la upatikanaji wa kuandaa mkutano unaowezekana. Sasa kuna mazungumzo ya maeneo mengine yanayowezekana, kama vile Geneva. Kwa hali yoyote, sio muhimu ambapo mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine ambayo sisi sote tunatumaini yatafanyika. Kilicho muhimu zaidi ni kwamba mazungumzo haya yaweze hatimaye kuanza, kwa sababu ni haraka kusitisha vita. Kwanza kabisa, mapatano ni ya dharura, kukomesha uharibifu, miji iliyoharibiwa, raia wanaopoteza maisha. Na kisha ni dharura kufikia amani iliyotulia, ya haki na ya kudumu, kwa hiyo iliyokubaliwa na kuafikiwa na pande zote mbili.

Neno amani limesikika kutoka dakika za kwanza kabisa kwenye midomo ya Papa mpya, siku ya kuchaguliwa kwake.

Ndio, Leo XIV anaendelea kwa nguvu baada ya watangulizi wake. Nilivutiwa na ukweli kwamba katika Sala yake ya Kwanza ya Malkia wa Mbingu kutoka katikati ya Dirisha la Kanisa Kuu la Vatican, yaani, mahali ambapo Papa Francisko alikuwa amewabariki waamini kwa mara ya mwisho, akizungumzia amani na upokonyaji silaha - Papa Leo alirudia maneno ya Mtakatifu Paulo VI katika Umoja wa Mataifa: “kamwe vita tena!" Papa na Vatican nzima wamejitolea kujenga amani na kukuza kila mpango wa mazungumzo na majadiliano.

Kuna wale wanaozungumza juu ya "kujipendekeza" iliyofanywa upya Vatican kwenye jukwaa la ulimwengu ...

Ni afadhali nirejee maneno mazito ya Leo XIV katika Mahubiri ya misa na Makardinali katika Kikanisa cha Sistine na katika mahubiri ya Misa kwa ajili ya mwanzo wa Upapa wake: “lazima tutoweke kwa sababu mhusika mkuu ni Kristo, Wakristo hawajisikii kuwa bora kuliko wengine bali wanaitwa kuwa “chachu kidogo katika unga,”,kushuhudia upendo, umoja na amani. Hapa, badala ya kuongelea "kujipendekeza” ningependelea kujumuisha pia mipango ya kidiplomasia katika muktadha huu wa huduma kwa amani na udugu.

Akikutana na waandishi wa habari, Papa Leo aliomba "mawasiliano tofauti." Je, kuna pia "vita vya maneno"?

Waandishi wa habari na wawasilianaji kwa ujumla zaidi hufanya kazi ya thamani, hata ya thamani zaidi wakati wa vita. Papa aliomba mawasiliano ambayo "hayajavaliwa na maneno ya uchokozi" na "hayatenganishi kamwe utafutaji wa ukweli na upendo ambao lazima tuutafute kwa unyenyekevu." Hata maneno yanaweza kuwa vyombo vya vita, au yanaweza kutusaidia kuelewana, mazungumzo, kutambuana kama ndugu. Amani huanzia kwa kila mmoja wetu na tumeitwa kuijenga kuanzia jinsi tunavyowasiliana na wengine. Kama Papa Leo alivyoeleza, lazima "tukatae dhana ya vita" pia katika mawasiliano.

Juu ya suala la kutafuta ukweli: katika siku za mwisho za Papa Francisko hadi siku zilizotangulia Mkutano wa Uchaguzi(conclave,) kulikuwa na maoni juu ya matendo ya siku za nyuma ya Wakuu mbalimbali wa Mabaraza ya Curia Romana kuhusiana na ripoti walizopokea za kesi za unyanyasaji. Je, zilichambuliwa?

Kuhusiana na maoni na uvumi juu ya hatua za baadhi ya Wakuu wa Mabaraza ya Curia Romana, kuhusu ripoti za kesi za unyanyasaji wakati walipokuwa maaskofu wa majimbo, uchunguzi uliofanywa na mamlaka husika, kupitia uchunguzi wa lengo na takwimu  ya maandishi, umebaini kuwa kesi hizo na normam iuris, yaani, kwa mujibu wa kanuni za sheria  zinazotumika, na zilitumwa na maaskofu wa majimbo ya wakati huo kwa Jimbo lenye uwezo kwa ajili ya uchunguzi wao na tathmini ya mashtaka. Ukaguzi uliofanywa na mamlaka husika haujapata kabisa ukiukwaji wowote katika matendo ya maaskofu wa majimbo.

Papa mpya, akichukua jina la Leo, anajiweka katika mwendelezo na Papa wa Rerum Novarum: mwishoni mwa karne ya kumi na tisa kulikuwa na mapinduzi ya viwanda, leo hii tunaishi wakati wa mapinduzi ya kidigitali na changamoto ambazo akili ya Nunde  inaleta. Je, tunawezaje kukabiliana na changamoto hizi?

Tunangoja tafakari ambayo Mrithi wa Petro atataka kufanya juu ya hili. Ninaamini kwamba njia sahihi si ile ya kukubalika bila kukosolewa wala ile ya kufanya uvumi. Uwezekano wa hali ya juu na wa utendakazi wa hali ya juu ambao teknolojia inatupatia lazima ubaki kuwa zana na utumike kwa manufaa kila wakati, bila kusahau kamwe kwamba hatuwezi kutawaliwa kwa mashine maamuzi ambayo yanahusu maisha au kifo cha binadamu. Ni lazima tuwe waangalifu ili kuepuka - kama kwa bahati mbaya wakati mwingine hutokea - kwamba akili ya dijitali na kwa hivyo pia akili nunde hutumiwa kama zana ya propaganda kushawishi maoni ya umma na ujumbe wa uwongo. Leo XIV, akikumbuka waandishi wa habari waliofungwa, alizungumza juu ya ujasiri "wa wale wanaotetea utu, haki na haki ya watu kufahamishwa, kwa sababu watu walio na habari ndio tu wanaweza kufanya uchaguzi huru."

27 Mei 2025, 15:22