ÐÓMAPµ¼º½

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Romanus Mbena kuwa Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, uteuzi huu unaanza tarehe Mosi Juni 2025. Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Romanus Mbena kuwa Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, uteuzi huu unaanza tarehe Mosi Juni 2025. 

Papa Leo XIV Amemteua Mons. Romanus Mbena Kuwa Mkuu wa Ofisi ya Huduma ya Upendo

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Romanus Mbena kuwa ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ambaye hadi kuteuliwa kwake amekuwa akihudumu kama Afisa Mshauri wa Balozi za Vatican ngazi ya kwanza na Mhudumu katika masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Monsinyo Romanus Mbena alipadrishwa kunako mwaka 1992 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Morogoro na kuanza utume wake katika Diplomasia mwaka 1995.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma ya Upendo, ambalo pia huitwa, Ofisi ya Misaada ya Kitume, ni kielelezo cha pekee cha huruma na upendo wa Mungu, kwa kutoa upendeleo wa pekee kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii; watu wanaohitaji kuonjeshwa huruma na upendo kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye katika hali ya umaskini au mahitaji mengine ambayo Baba Mtakatifu binafsi anaamua juu ya misaada itakavyogawiwa. Baraza hili liko chini ya Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Kipapa anayeshirikiana na Mabaraza mengine, ili kuhakikisha kwamba, misaada inawafikia walengwa, kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, Mchungaji mkuu wa Kanisa la Kiulimwengu kwa ajili ya maskini, watu wanaosukumiziwa pembezoni mwa jamii au katika matukio ya majanga makubwa.

Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo   (@Mariusz Krawiec.)

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Romanus Mbena kuwa ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ambaye hadi kuteuliwa kwake amekuwa akihudumu kama Afisa Mshauri wa Balozi za Vatican ngazi ya kwanza na Mhudumu katika masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Romanus Mbena ni Padre wa Jimbo Katoliki Morogoro, Tanzania. Uteuzi huu unaanza mara moja tarehe 1 Juni 2025. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Romanus Mbena alipadrishwa kunako mwaka 1992 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Morogoro na mwaka 1995 akajiunga na huduma ya Diplomasia ya Kanisa. Tangu wakati huo amehudumu kwenye Balozi za Vatican nchini Zambia, Panama, Ghana Trinidad na Tabago, Sudan, Ethiopia, India na Albania.

Mons. Romanus Mbena
30 Mei 2025, 16:59