Papa Leo XIV amemteua Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha ya kitawa na kazi za kitume!
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV, alhamisi tarehe 22 Mei 2025 amemteua Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume, Mweshimiwa Sr Tiziana Merletti,ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika la Wafransiskani Maskini.
Wasifu wake
Sr. Merletti alizaliwa tarehe 30 Septemba 1959 huko Pineto (TE), Italia. Kunako 1986 alifunga nadhiri za kwanza katika Taasisi hiyo ya Wafransiskani Masikini.
Mnamo mwaka 1984 alipata digrii ya sheria katika Chuo Kikuu Huria cha Abruzo cha (“Gabriele d’Annunzio” huko Teramo, na kunako 1992, alipata Udkatari wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma. Tangu 2004 hadi 2013 alikuwa Mkuu wa Shirika lake la kitawa. Hadi uchaguzi wake ni Profesa katika Kitengo cha Sheria za Kanoni za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum, Roma na kushirikiana katika masuala ya kisheria na Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika kimataifa.