Papa Leo XIV amefanya teuzi mpya
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 19 Mei 2025, amefanya teuzi mbali mbali: Amemteu Kansela wa Taaisisi ya Kipapa la Taalimungu, ya (Yohane Paulo II) kwa ajili ya Sayansi ya Ndoa na Familia, Kardinali Baldassare Reina, Makamu wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya Jimb la Roma na Kansela wa Chuo cha Kipapa Laterano.
Baba Mtakatifu amemteua Kardinali François-Xavier Bustillo, O.F.M. Conv., Askofu Mkuu wa Ajaccio, kuwa mwakilishi wake maalum katika hitimisho la Maadhimisho ya miaka 350 ya kutokewa kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu kwa Mtakatifu Margherita Maria Alacoque, itakayofanyika katika madhabahu ya Paray-le-Monial, tarehe 27 Juni 2025 huko Ufaransa.
Baba Mtakatifu Leo XIV aidha amemteua Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Mheshimiwa Padre Avelino Chicoma Bundo Chico, S.I., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Afisa wa Ofisi hiyo ya Curia Romana.