"Nyuso za Injili,"Papa Francisko anazungumza kuhusu Mtakatifu Yosefu
Sehemu ya kumi na tano kati ya 18 inayounda "Nyuso za Injili," iliyopendekezwa tena na Vatican News katika kipindi hiki cha Pasaka,sura ya Yosefu,seremala kutoka Nazareti na mume wa Maria.
Vatican News
“Mtakatifu Yosefu alitii na kuamini baada ya ile ndoto ambayo ilimueleza kinachoendelea. Ilibidi akabiliane na mambo mawili: ubaba na fumbo. Alifanya hivyo kwa ukimya, bila kusema neno lolote, katika Injili hakuna neno lililosemwa na Yosefu:” hivi ndivyo Papa Francisko anavyozungumza kuhusu baadhi ya matukio ya Yesu katika kipindi hicho, kilichotangazwa katika kipindi kikuu cha Dominika ya Pasaka 2022 kwenye Rai Uno,(Italia) iliyosimamiwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa kushirikiana na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na Rai Utamaduni. Waandishi wa mfululizo huo ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, mwelekeo na upigaji picha uliratibiwa na Renato Cerisola, muziki asilia umeundwa na Michelangelo Palmacci.
23 Mei 2025, 11:47