ĐÓMAPµĽş˝

 Padre Costa de Beauregard alitangazwa kuwa Mwenyeheri. Padre Costa de Beauregard alitangazwa kuwa Mwenyeheri.  (© Diocèses de Savoie)

Kutangazwa Mwenyeheri Padre Camille Costa,Verny:Mfano wa elimu ya vijana wote!

Tarehe 17 Mei 2025,Padre Savoyard wa karne ya 19,aliyejitolea katika elimu ya watoto yatima na waliotengwa amekuwa wa kwanza kutangazwa kuwa mwenyeheri kwa Papa Leo XIV.Askofu Mkuu wa Chambéry:Padre Camille ni kielelezo cha utendaji katika uso wa mateso.Kuna shauku inayokwenda zaidi ya jiji la Chambéry,zaidi ya Savoy,hata nje ya Kanisa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Wakati wa Misa nilihisi uwepo wa nguvu wa kiroho wa Papa Francisko, ambaye anatusindikiza kutoka Mbinguni. Katika mwelekeo huu wa ushirika wa watakatifu ninakumbuka kwamba jana huko Chambéry, Ufaransa, Padre Camille Costa de Beauregard alitangazwa kuwa Mwenyeheri, aliyeishi kati ya mwisho wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, shahidi wa upendo mkuu wa kichungaji.” Ndivyo Baba Mtakatifu Leo XIV alisema wakati wa Sala ya  Malkia wa Mbingu, Dominika tarehe 18 Mei 2025 katika siku ya Misa ya kuanza kwa Huduma ya Mfuasi wa Mtume Petro akiwageukia waamini zaidi ya miambili hamsini elfu waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Misa hiyo ya kutangazwa mwenyeheri kwa hiyo ilikuwa Jumamosi tarehe 17 Mei 2025 saa 9 alasiri ambapo Balozi wa Vatican  nchini Ufaransa, Askofu Mkuu Celestino Migliore, aliongoza  Ibada hiyo akimwakilisha Papa, kwa  Padre huyo wa Savoyard wa karne ya 19, aliyejitolea kuwalea watoto yatima na Mwenyeheri wa kwanza  kutangazwa wakati wa upapa wa Papa Leo XIV.

Mwenyeheri wa  kwanza wa Papa  Leo XIV

Maadhimisho hayo yalifanyika alikozaliwa Camille, Chambéry, katika Milima ya Ufaransa kunako 1841, katika familia yenye heshima na ushawishi na akakulia humo. Katika Kanisa Kuu ambalo Misa ya kumtangaza mwenyeri lifanyika, kwake yeye akiwa na umri wa miaka 20 aligundua tena imani yake na kuamua kuwa Padre. Kisha alitumwa Roma kukamilisha mafunzo yake ya kikanisa. Alisoma katika seminari ya Kifaransa jijini Roma na kupewa daraja la upadre katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano. alikumbusha Askofu Mkuu Verny. Hata hivyo mnamo Aprili 2025, waamini majimbo matatu ya Savoy (Chambéry, Maurienne na Tarentaise) walifanya hija mjini Roma kwa kufuata nyayo za siku zijazo za mwenyeheri. Kisha kikatokea kifo cha Papa Francisko kunako tarehe 21 Aprili 2025 ambacho kilitia shaka juu ya kutangazwa kuwa mwenyeheri. Lakini Papa Leo XIV alithibitisha maadhimisho yake , yakiidhinisha hati iliyotolewa tarehe 14  Machi 2024 kuendelea.

Historia

Historia yake kwa kukataa kuingia katika Chuo cha Waheshimiwa cha Kikanisa, ambacho kingemhakikishia kazi nzuri ya kidiplomasia ya Vatican, Camille alirudi Chambéry na kuwa makamu wa Kanisa kuu. Miezi miwili baadaye, mnamo Agosti 1867, ugonjwa wa kipindupindu ulikumba jiji hilo kwa nguvu. Akikabiliwa na mateso ya watoto yatima, “Camille alisimama kidete  na kuitikia.” Kwa kutumia urithi wa familia yake tajiri, alianzisha Nyumba ya yatima ambapo aliwakaribisha yatima na kuwafundisha biashara ya kilimo. Aliongoza kazi hii hadi kifo chake mwaka 1910, akiwa na umri wa miaka 69.

 â€śInatia moyo sana kufikiri kwamba mtu yeyote anaweza kufuata kielelezo cha Camille anapokabili mateso,” alisisitiza Monsinyo Verny, akinukuu maneno ya Yesu, kutoka katika Injili ya Mathayo: “Wakati wowote mlipomtendea mmoja wa walio wadogo zaidi wa hawa ndugu zangu mambo haya, mlinitendea mimi.” Mwenyeheri  mpya anawakilisha kielelezo cha utakatifu kwa nyakati zetu. Kwanza kabisa kwa sababu alidhulumiwa akiwa kijana: “Alipokuwa katika shule ya bweni, hakuwa na furaha sana, kwa hiyo yuko karibu na watoto wanaoteseka vivyo hivyo leo.” Pia, kwa mtazamo wake wa elimu: "Katikati palikuwa na uhusiano wa kuaminiana kati ya waelimishaji na vijana waliokaribishwa, uti wa mgongo wa elimu." Leo, huko Bocage inaendelea na misheni yake ya kielimu kama kituo cha kilimo na msingi kama Mfuko wa  Bocage, kiachosimamiwa na Wataw wa Mtakatifu Dono  Bosco.

Mwenyeheri na mkutano na Don Bosco huko Torino

Wakati ujao wa Mwenyeheri  na Don Bosco walikutana huko Torino mnamo 1879 na ufundishaji wao unafanana sana. "Wanafanana kidogo na binamu," alitania Askofu  Verny. "Ni kichocheo kwa Kanisa kuendelea kujitolea kwa elimu, heshima, ushujaa wa kila mtu na kuwa na mtazamo mzuri ambao Camille aliweza kutoa ili kuwapa ujasiri vijana na kuwafanya wawajibike." Urithi wa Camille Costa de Beauregard unavuka mipaka ya Chambéry, Savoy na hata Ufaransa. Mahujaji zaidi na zaidi wanakuja jijini kufuata njia "katika nyayo za Camille", wengine hata wakitoka mbali sana. Katika Mwaka huu wa Jubilei 2025, sisi sote ni mahujaji wa matumaini: kutangazwa kuwa Mwenyeheri si mahali pa kuwasili, bali ni hatua ya kuondoka ili kuimarisha matumaini yetu katika Mwaka Mtakatifu na zaidi", alihitimisha  Askofu Mkuu Verny.

Utangazaji wa Mwenyeheri mwingine 17 Mei, huko Estonia

Utangazaji mwingine, ule wa Askofu Eduard Profittlich, pia ulipaswa kufanyika Jumamosi tarehe Mei 17 huko Estonia, lakini uliahirishwa kwa sababu za vifaa. Mjesuiti wa Ujerumani, Askofu mkuu wa Adrianople, msimamizi wa kitume wa Estonia, alikamatwa na kuhamishwa hadi Urusi ambapo alipitia mateso mengi na, kuhukumiwa kifo, alikufa kabla ya utekelezaji wa hukumu kutokana na mateso ya gerezani, tarehe 22 Februari 1942.

Mwenyeheri mpya
18 Mei 2025, 17:55