ÐÓMAPµ¼º½

Mpango wa Taasisi ya Muziki Mtakatifu

Hebu tuimbe pamoja na Papa

Vatican News

Padre Robert Mehlhart, Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Muziki Mtakatifu (PIMS),alielezea mpango huo: "Hebu tuimbe pamoja na Papa," ambao ni mfululizo wa mafunzo mafupi ya elimu ya video  yaliyoshirikishwa kwenye mitandao ya kijamii ili kuwasaidia watu wa Mungu kuimba pamoja na Papa wakati wa sherehe kuu za kiliturujia.

Hii ni kufanya urithi wa nyimbo za Gregorian kupatikana, lugha ya muziki ya ulimwengu wote na ya kiroho ambayo inaruhusu ushiriki hai katika liturujia. "Ni rahisi sana," mkuu wa Taasisi ya Muziki aliviambia vyombo vya habari vya Vaticani kuwa, "Mimi huimba sehemu za Misa na kisha  sehemu  kuu  ya mwisho tunaimba pamoja na Papa. Nilifikiri kwamba kwa njia hii watu wanasali kweli kwa sababu wanaingia katika mazingira haya ya sala na hata wale ambao hawatakuwepo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro wanaweza kushiriki kwa sababu watajua jinsi ya kuimba na Papa."

Taasisi ya Kipapa ya Muziki Mtakatifu ina wanafunzi 153 kutoka nchi 44: 10 kati yao walikuwa katika kwaya iliyoongoza Ibada ya Misa Takatifu ya mwanzo wa Upapa wa Papa Leo XIV,  Dominika tarehe 18 Mei 2025.

Baba Mtakatifu  Leo XIV
Baba Mtakatifu Leo XIV   (@Vatican Media)
20 Mei 2025, 12:28