Kardinal Dziwisz:Mtakatifu Yohane Paulo II aliokolewa na Bikira Maria
Karol Darmoros,Krzysztof Bronk na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwanzoni mwa maadhimisho ya misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 13 Mei 2025 , saa 12 kamili jioni masaa ya Ulaya, Kardinali Stanislaw Dziwisz alimtaja Papa mpya Leo XIV kwa kuoesha kwamba, kuchaguliwa kwake kulifanyika katika siku kuu ya Mama Yetu wa Rozari wa Pompei, na kwa hiyo Kardinali huyo alipenda kukabidhi upapa mpya kwa maombezi ya Bikira Maria na Mtakatifu Papa Yohane Paulo II. Askofu Mkuu Mstaafu wa Krakow wakati wa mahubiri yake alisisitiza kwamba "miezi michache iliyopita imewaacha waamini kuwa karibu zaidi na Kanisa na mambo yake."
Kardinali Dziwisz alikumbuka enzi za ugonjwa na kuendelea kupona kwa Baba Mtakatifu Francisko na sala ya Kanisa kumsindikiza Papa kuwa: "Tulipokea baraka zake za mwisho siku ya Dominika ya Ufufuko, na siku iliyofuata tuliguswa na habari za kufariki kwake katika umilele. Ilikuwa ni kwa huzuni kwamba tuliagana na Papa, tukimshukuru Mungu kwa miaka kumi na miwili ya huduma ya Kanisa kwa ulimwengu."
Askofu Mkuu Mstaafu wa Krakow aliendelea kuongeza kwamba: "kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Leo XIV ni zawadi ya Kristo Mfufuka kwa ajili ya Kanisa Lake." Na kwa kuthibitisho wa Mungu asemaye kuwa "Nitawapa ninyi wachungaji waupendezao moyo wangu.†Zaidi ya hayo alisema kwamba "Kanisa la Poland litakumbuka daima kwamba Papa mpya alichaguliwa tarehe 8 Mei ambapo Mama Kanisa anafanya Siku kuu ya Mtakatifu mlinzi mkuu wa Poland, Mtakatifu Stanislaus, Askofu na Mfiadini."
Kurushwa kwa risasi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Kardinali StanisÅ‚aw Dziwisz alidokeza kwamba muda kabla ya kuanza rasimi utume wa Upapa wa Papa Leo XIV unakwenda sambamba karibu na kumbukumbu ya miaka 44 ya jaribio la mauaji ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili. "Maadui wa Kristo na Kanisa walitaka kumnyima uhai Mchungaji ambaye, kwa kuhubiri Injili ya upendo na amani, alirejesha matumaini kwa watu waliokandamizwa na watumwa waliokuwa wakitamani ukweli na uhuru", alisema Katibu wa zamani wa Papa Karol Wajytla na shahidi aliyeshuhudia mauaji hayo. Kardinali Dziwisz alikumbuka kwamba, alisindikizana na Baba Mtakatifu aliyejeruhiwa katika njia yake ya kwenda kwenye Hospitali ya Gemelli na kumpatia Sakramenti ya mpako wa ugonjwa: “Nilikesha baada ya upasuaji huo wa saa nyingi na kusali kwa ajili ya muujiza wa kuokoa maisha yake, kwa sababu alikuwa akihitajika na Kanisa na dunia nzima.â€
Msamaha mara moja
Kardinali Dziwisz alisisitiza kuwa, akiwa amejeruhiwa vibaya sana, Papa hakujifikiria yeye mwenyewe bali, aliombea Kanisa na ulimwengu kam: “Hatapendezwa na nani aliyefyatua risasi hizo, hata kama angetamka maneno ya msamaha kwa ‘ndugu’ kama anavyomwita muuaji.†Kardinali zaidi ya hayo alionesha kwamba, wakati huo Baba Mtakatifu alilitumikia Kanisa kwa mateso yake na alifahamu kwamba waamini wanaomba kwa ajili yake pia, "kama vile Kanisa la kwanza lilivyoomba kwa ajili ya Petro, kuwekwa gerezani na kufungwa kwa minyororo miwili." Dziwisz aliongeza kuwa Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa na hakika kwamba anadaiwa kuishi kwa Bikira Maria aliyebarikiwa, tangu Mei 13 aliadhimisha kutokea kwake huko Fatima: "Siku hiyo (...) alizuia mipango ya muuaji na wale waliomtuma kumuua."
Kuhubiri Habari Njema
Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu Mstaafu wa Krakow alihimiza mtazamo wa Maria, ambaye alitoa maisha yake katika huduma ya Mungu na Mwanawe. Katika muktadha huo alibainisha kwamba, njia ya kusikiliza na kuhifadhi Neno la Mungu inapaswa kuwa mchango wa waamini katika maisha na utume wa Kanisa la kisasa, kwa kuhubiri Habari Njema kwa ulimwengu wa sasa usio na utulivu. Zaidi ya hayo, Kardinali Dziwisz alirejea maneno ya Papa Leo XIV kutoka kwenye mahubiri yake ya kwanza, Baba Mtakatifu alipozungumza kama vile kuhusu kudhihaki imani na kuichukulia kama upuuzi, huku watu wakitafuta dhamana nyinginezo, kama vile teknolojia, pesa, mafanikio, mamlaka, au raha. Kama Kardinali Dziwisz alivyoonyesha, Ulimwengu huu, hata hivyo, unafanya utume wa Kanisa kuwa wa haraka zaidi kwani, kama Baba Mtakatifu anavyoona, ukosefu wa imani mara nyingi huchochea mchezo wa kweli. Katibu wa zamani wa Papa alihimiza sala kwa ajili ya Papa mpya, akiomba neema ya neema ya Mungu kwa ajili yake, ili aweze, kama Petro wa leo, kuliongoza Kanisa na kutusaidia sisi sote kutoa agano hai la imani yetu."