ĐÓMAPµĽş˝

2025.05.20 Kardinali Parolin amepokea tuzo kutoka Mfuko wa "Tuzo ya Njia ya Amani 2025." 2025.05.20 Kardinali Parolin amepokea tuzo kutoka Mfuko wa "Tuzo ya Njia ya Amani 2025."  (Terza Loggia )

Kard.Parolin apokea tuzo ya amani:kwa huduma ya Papa na Ulimwengu wa haki zaidi

Tarehe 19 Mei,huko New York,Kardinali Parolin alipokea tuzo kutoka Mfuko wa"Path to Peace,"huku akisema kuikubali kwa niaba ya Sekretarieti ya Vatican ambayo inafanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kuhamasisha haki katika ulimwengu.Katika hotuba yake alikumbusha hotuba za Mapapa wa mwisho ambao wameonesha njia ya amani ya kupitia hekima,uvumilivu,ujasiri na ubunifu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

"Nimefurahi sana kupokea Tuzo ya  Njia ya Amani na ninaikubali kwa niaba ya Vatican na, zaidi ya yote, kwa niaba ya Sekretarieti ya Vatican ambayo inafanya kazi bila kuchoka kwa niaba ya Papa wa Roma kukuza amani na haki katika ulimwengu wetu." Kwa maneno hayo mnamo Jumatatu tarehe 19 Mei 2025  Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiwa huko New York alipokea tuzo iliyotolewa kwake na Mfuko wa ( Path to Peace Foundation) Njia ya Amani , ulioanzishwa mwaka 1991 na Askofu Mkuu wa wakati huo Renato Raffaele Martino, alipokuwa Mwakilishi wa  kudumu wa Vatican  kwenye Umoja wa Mataifa. "Heshima iliyotolewa jioni hii inapita ubinafsi na inajumuisha roho ya ushirikiano ambayo ni msingi wa utume wetu wa Vatican katika ulimwengu unaolilia uponyaji na upatanisho," alisema Kardinali Parolin. Na alikumbuka katika suala hili kwamba kiini cha utume wa Vatican ni njia iliyofuatiliwa na Warithi mbalimbali wa Kharifa wa mtume Petro kwa ajili ya ulimwengu usio na migogoro.

Kardinali Parolin apokea Tuzo ya njia  ya Amani
Kardinali Parolin apokea Tuzo ya njia ya Amani

Katika mwaka huu wa 2025 ambapo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka sitini ya ziara ya Mtakatifu Paulo wa Sita katika Umoja wa Mataifa, kumbukumbu ya miaka thelathini ya ziara ya pili ya Mtakatifu Yohane Paulo II, na kumbukumbu ya miaka kumi ya hotuba ya Papa Francisko kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Kardinali Parolin alisisitiza jinsi "kila Papa, kwa wakati wake, ametoa mwanga juu ya njia ya amani na kuvuka mipaka ya dunia." Kardinali Parolin  alikumbuka maneno ya Mapapa mbalimbali, akianza na Papa Montini (Paulo VI) ambaye alisema “kwa uwazi wa kiunabii” kunako  1965 kwamba amani ya kudumu lazima “isimike mizizi katika upyaisho wa kiroho na kiadili.” Maneno haya leo hii yanahifadhi uharaka wake, yakikumbusha kwamba maendeleo ya kiteknolojia bila maendeleo ya kiadili yanaacha ubinadamu katika hatari .”

Kardinali Parolin kisha alitoa mfano wa ombi la Papa WojtyĹ‚a mnamo 1979 kwa ubinadamu kukabiliana na uwezo wake wa kutenda mema na ukatili usioelezeka, akiakisi utu wa ndani na usiovunjwa wa kila mtu. Papa Yohane Paulo wa Pili alichota kutokana na uzoefu wake mwenyewe wa utawala wa kiimla na vita,” akieleza Maangamizi Makubwa ya kimbari ya  Vita vya Pili vya Ulimwengu kuwa si tu kama matukio ya kihistoria, bali kama changamoto za kimaadili zinazoendelea kudai itikio letu.” Na tena Katibu wa Vatican alikumbusha maneno ya Papa  Benedikto XVI mwaka 2008, alipothibitisha "ukweli wa ulimwengu wote na usiobadilika ambao haki za binadamu zimejengwa na kwamba ulinzi wa utu wa binadamu lazima uchukuliwe jukumu la pamoja la jumuiya nzima ya kimataifa.”

Kardinali Parolin huko UN katika hafla ya kukaribisha uchaguzi wa Papa Leo XIV
Kardinali Parolin huko UN katika hafla ya kukaribisha uchaguzi wa Papa Leo XIV

Pamoja na msisitizo wa Papa  (Hayati Papa Francisko)  kunako 2015 kuhusu "muunganisho kati ya ulinzi wa mazingira na haki ya kijamii na ukosoaji wa usumbufu wa "utamaduni wa kutupa. Na sasa,  aliongeza  tamaduni hii inaendelea" na Papa Leo XIV ambaye katika maneno yake ya kwanza kama Papa alitoa wito wa "kupokonywa silaha na kupokonya maangamizi, " amani kama "nguvu chanya" katika ulimwengu ulioharibiwa na migogoro na migawanyiko.” Katibu wa Vatican pia alibainisha chaguo la jina la Papa mpya, ambaye alitaka kusisitiza umuhimu wa mafundisho Jamii ya Kanisa katika muktadha wa maendeleo ya kisasa ya teknolojia ambayo yanaathiri utu na haki ya binadamu.


Katika muktadha huo, Kardinali alisisitiza kwamba tuzo aliyopewa ni utambuzi wa uungaji mkono wa Vatican,  ingawa wakati mwingine ni muhimu  wa  uhusiano na Umoja wa Mataifa, na pia heshima kwa wale wote wanaomsaidia Papa katika utume wake. Kwa kuongezea kwamba njia ya amani lazima ipitiwe  kwa subira na ustahimilivu, kwa ujasiri na ubunifu" na kwamba "Mapapa wametuonesha njia." Zaidi ya hayo, Umoja wa Mataifa lazima uendelee kujipyaisha, si tu kitaasisi, bali pia kiadili na kiroho.” Athari za ahadi hii hazitaonekana “katika mikataba au maazimio” bali katika “mabadiliko ya moyo wa binadamu kuelekea haki zaidi, huruma na heshima kwa utu wa kila mtu,”na kwa njia hiyo Katibu wa Vatican alihitimisha, akitoa shukrani kwa Mfuko wa  Path to Peace Njia ya Amani  kwa kuunga mkono ujumbe wa Mwakilishi wa kudumu kwa Umoja wa Mataifa na ujumbe wa amani wa Vatican.

Tuzo kwa Kardinali Rugambwa
20 Mei 2025, 15:34