ĐÓMAPµĽş˝

2025.05.23 Askofu Mkuu  Ignazio Ceffalia, Balozi mpya wa Vatican nchini Belarus. 2025.05.23 Askofu Mkuu Ignazio Ceffalia, Balozi mpya wa Vatican nchini Belarus. 

Kard.Parolin:huduma ya Askofu ni zawadi kwa Kanisa lote!

Katibu wa Vatican aliadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ya kuwekwa wakfu kwa Mons.Ignazio Ceffalia,Balozi wa Vatican nchini Belarus tangu Machi 25.Kardinali anaamini kuwa Askofu atakabiliwa na huduma mpya kwa uhakika wa neema ya Mungu,licha ya changamoto za ndani za hali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi,lakini pia kidini kwa uhusiano na ndugu wa Kiorthodox na katika uso wa mvutano na vita vya kutisha vya Ukraine visivyoisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Huduma ya Askofu ni zawadi iliyokusudiwa kwa Kanisa zima ambayo ina maana kwamba mteule haishi tena kwa ajili yake mwenyewe, bali kwa ajili ya jumuiya nzima ambayo ameteuliwa kuwa. Haya ni maneno ya Kardinali Pietro Parolin akielezea utume wa Maaskofu kwa namna hii katika mahubiri yaliyotolewa tarehe 22 Mei 2025 wakati wa kuwekwa wakfu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwa Mons. Ignazio Ceffalia aliyeteuliwa tarehe 25 Machi 2025 iliyopita kuwa Balozi wa Kitume nchini Belarus.

Kuwekwa wakfu wa kiaskofu
Kuwekwa wakfu wa kiaskofu   (@Vatican Media)

Ni huduma ambayo Kardinali anaamini sana mteule huyo Askofu Mkuu Ceffalia atakabiliwa na uhakika wa msaada kutoka kwa Mungu licha ya changamoto za ndani za hali ya kisiasa na kijamii na kiuchumi, lakini pia ya kidini kwa uhusiano na ndugu zetu wa kiorthodoksi, na mbele ya mivutano ya kikanda na ya bara inayohusishwa na vita vya kutisha vinavyoendelea huko Ukraine, ambavyo kwa bahati mbaya bado haviishi. Kardinali Parolin kwa kutumia  nukuu kutoka kwa Mtakatifu Agostino, aliyetajwa hivi karibuni na Papa Leo XIV, alisema “kwenu ninyi mimi ni askofu, pamoja nanyi mimi ni Mkristo,”ilikuwa ni kutaka  kusisitiza jinsi huduma ya uaskofu ilivyo zawadi kutoka kwa Bwana kwa ajili ya kuujenga mwili wake, ambayo inahusisha kujitolea kusiko na kikomo, ili mteule asifikirie tena maslahi yake mwenyewe, bali ya manufaa ya wote.” Katibu wa Vatican kama mwakilishi wa Papa alishirikisha  "kwa namna ya pekee sana katika kujali Makanisa yote ambayo Maaskofu wanapaswa kutekeleza kwa mujibu kwa wajumbe wake wa Baraza la Maaskofu."

Kardinali Parolin
Kardinali Parolin   (@VATICAN MEDIA)

Katika mahubiri yake, alirejea uzoefu mbalimbali wa Monsinyo Ceffalia ambaye, baada ya kumaliza masomo yake, kuanzia mwaka wa 2006 na kuendelea alikuwa “nchini Ecuador, huko Strasbourg, katika utume wa kudumu wa Baraza la Ulaya, katika Sekretarieti ya Vatican kama afisa wa kitengo cha mahusiano na Mataifa, na hatimaye nchini Venezuela” ambako alihudumu kama Nuru ya kitume. Zaidi ya yote, misheni hii ya mwisho ilikuwa ngumu hasa kutokana na hali ya kisiasa na kijamii na kiuchumi ya nchi,” kadinali huyo anasisitiza, “ambamo, hata hivyo, mliweza kuona neema ya Bwana, ambaye kulingana na fundisho la kimapokeo la Kanisa haachi kamwe kukosa chochote kwa wale wanaofanya kazi fulani. Ili kukabiliana na mazingira yote na kuishi kikamilifu karama ya uaskofu, Katibu wa Jimbo anamsihi Askofu mkuu mpya kulinda zawadi ya Roho Mtakatifu anayokabidhiwa kwake kwa kuwekewa mikono.

Wakati wa kuwekwa wakfu wa kiaskofu
Wakati wa kuwekwa wakfu wa kiaskofu   (@VATICAN MEDIA)

Karama hii ya kudumu ya kiroho inawaka kama moto, lakini moto huu unaowaka haunjilishi wenyewe, unakufa ikiwa hautawekwa hai, alisisitiza Kardinali Parolin. Ili kuwa nuru ya ulimwengu na kuifanya nuru yako iangaze mbele ya watu, moto lazima uwashwe upya na itakuwa ni ahadi ya kila siku, kujitolea kwa maisha yako yote kama Askofu. Kardinali Parolini alimtia moyo pia apate msukumo kutoka kwa mtakatifu wake, Ignatius wa Antiokia kwamba “Askofu mwenye nguvu, mchungaji anayewaka bidii, waamini wake wamemfafanua kuwa mwamini wa moto, kama vile neno lenyewe la  jina lake linavyodokeza. Hata kifo chake cha kusikitisha cha kishahidi akiwa ameraruliwa vipande-vipande na wanyama wakali katika Colosseum , ni fundisho kwamba usione haya kumshuhudia Bwana wetu bali tuteseke pamoja na Mungu kwa ajili ya Injili, aliendelea Kardinali Parolin, akitoa mfano wa somo la kwanza la Misa lililotolewa katika usomaji wa Mtume Paulo kwa Timotheo.

Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu
Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu   (@VATICAN MEDIA)

Askofu lazima azingatie mantiki ya msalabalakini moyo wake umekusudiwa kuumbwa na moyo wa Kristo na kuendeleza ulimwenguni na kwa wakati muujiza wa upendo wa Yesu", anaendelea Katibu wa Jimbo, akinukuu hotuba ya Papa Paulo VI kwa maaskofu wa Italia mnamo 1973. Kiukweli ni nzuri, ya kusisimua, inayoweza kujaza maisha kuwa mjumbe, mtume na mwalimu wa udhihirisho wa Mwokozi wetu Yesu Kristo". Kwa Kardinali Parolini ilikuwa ni furaha na uhakika huu wa Yesu mfufuka anayemlinda kila mtu unaakisiwa pia katika kauli mbiu ya kiaskofu iliyochaguliwa na Monsinyo Ceffalia isemayo : “Ego autem in te speravi”, “Lakini mimi nimekutumaini wewe, Ee Bwana.”

Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu
Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu   (@VATICAN MEDIA)

Misa hiyo katika Kanisa kuu ni wimbo wa shukrani na sauti mbili: kutoka katika Kanisa la Kilatini, lakini pia kutoka katika Kanisa Katoliki la Kigiriki-Byzantine la Waalbania nchini Italia, ambalo Askofu mkuu mpya ni mzaliwa wa Palermo mwaka  1975 na kuwekwa wakfu wa Upatriaki wa Piana ya Albanesi mnamo mwaka 2003. Kwa hakika, liturujia iliwekwa alama kwa baadhi ya nyimbo kutoka katika mapokeo haya, na pia kwa taratibu za kuwekwa wakfu maaskofu: upako wa kristo na kisha utoaji wa Injili, pete ya maaskofu, mitra na fimbo ya kichungaji. Maaskofu mbalimbali walikuwepo, wakiwemo wale wa Kanisa Katoliki la Ugiriki-Byzantine, na Kardinali Francesco Montenegro, msimamizi wa kitume wa Piana ya Waalbania, na Askofu Mkuu Paul Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, walishiriki wa misa hiyo ya kuwekwa wakfu.

Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu
Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu   (@VATICAN MEDIA)
Mahubiri Kardinali Parolin
23 Mei 2025, 09:24