ÐÓMAPµ¼º½

Ajali ya moto imesababisha vifo vya watu 59, huku kati yao 35 wakiwa wametambuliwa tayari. Zaidi ya watu 155 wamejeruhiwa vibaya sana, kutokana na moto uliozuka usiku wa kuamkia Dominika tarehe 16 Machi 2025. Ajali ya moto imesababisha vifo vya watu 59, huku kati yao 35 wakiwa wametambuliwa tayari. Zaidi ya watu 155 wamejeruhiwa vibaya sana, kutokana na moto uliozuka usiku wa kuamkia Dominika tarehe 16 Machi 2025.   (ANSA)

Vijana 59 Wafariki Dunia Kwa Ajali ya Moto Macedonia ya Kaskazini

Serikali ya Macedonia ya Kaskazini imetangaza siku saba za maombolezo kufuatia ajali ya moto uliotokea kwenye klabu ya usiku ya "Club Pulse" huko Kocani, Macedonia Kaskazini na kusababisha vifo vya watu 59, huku kati yao 35 wakiwa wametambuliwa tayari. Zaidi ya watu 155 wamejeruhiwa vibaya sana, kutokana na moto uliozuka usiku wa kuamkia Dominika tarehe 16 Machi 2025. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa hii na ametuma salam za rambirambi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Serikali ya Macedonia ya Kaskazini imetangaza siku saba za maombolezo kufuatia ajali ya moto uliotokea kwenye klabu ya usiku ya "Club Pulse" huko Kocani, Macedonia Kaskazini na kusababisha vifo vya watu 59, huku kati yao 35 wakiwa wametambuliwa tayari. Zaidi ya watu 155 wamejeruhiwa vibaya sana, kutokana na moto uliozuka usiku wa kuamkia Dominika tarehe 16 Machi 2025. Vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo vinawashikilia watu 15 wanaotuhumiwa kuhusika na janga hili la moto. Takriban watu 1,500 wengi wao wakiwa vijana wa kizazi kipya walikuwepo kwenye tamasha katika klabu hiyo ya usiku wakati moto huo ulipozuka. Hawa ni vijana ambao walikuja kushuhudia wasanii wa muziki wa kufoka foka maarufu hip-hop waitwao Dnk. Moto huo ulisababishwa na fataki zilizopigwa wakati wa onyesho la Dnk.

Ajali ya moto imesababisha watu 59 kufariki dunia huko Macedonia ya Kaskazini
Ajali ya moto imesababisha watu 59 kufariki dunia huko Macedonia ya Kaskazini   (AFP or licensors)

Ukumbi ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 700, lakini taarifa inaonesha kwamba, kulikuwa na takribani watu 1500. Waandaaji wa tamasha hili la muziki hawakuwa na leseni na kwamba, wanashikiliwa kwa kwa tuhuma za rushwa na ubadhilifu. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa ya janga hili la moto. Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu Kiro Stojanov wa Jimbo Katoliki la Skopje, anamwomba, awafikishie salam zake za rambirambi watu wote walioguswa na kutikiswa na janga hili la moto na kwamba, yuko karibu kwa njia ya sala na sadaka yake na wale wote waliojeruhiwa. Anawaombea raha na mwanga wa milele wale wote waliopoteza maisha katika ajali hii. Anawaombea watu wa Mungu nchini Macedonia ya Kasikazini faraja na kitulizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma na mapendo katika kipindi hiki cha majonzi mazito. Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko anatoa baraka zake za kitume.

Ajali ya Moto
17 Machi 2025, 10:05