Askofu Mkuu Gallagher:Gaza ibaki kuwa nyumba ya Wapalestina
Vatican News
Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa katika sehemu ya kwanza ya mahojiano marefu na jarida la "Marekani", lililoanzishwa na Jumuiya ya Yesu nchini Marekani, iliyotolewa hivi karibuni baada ya kushiriki katika Mkutano wa kila mwaka wa Usalama huko Munich nchini Ujerumani, alisisitiza msimamo wa Vatican wa kupata suluhisho la serikali mbili. “Licha ya uharibifu na magofu ambayo yako, Gaza ni nyumba za Wapalestina ambao kwa vizazi vilizaliwa na kuishi huko na ambao katika ardhi hiyo wanataka kukaa, kujenga upya maisha yao na hatuwezi kwenda kinyume haya yote.” Akijibu swali kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwapa makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza mahali pengine, alikumbusha kuwa ni wangapi kati yao au babu zao wa karibu ambao tayari wamelazimishwa kuondoka na mali waliyokuwa nayo katika maeneo mengine ya Nchi Takatifu. "Si sawa kusema kwamba wao ni shida. Wao ni watu na kwa hivyo lazima watendewe, heshima kwao na kuelekea hadhi yao kama wanadamu, bila kusahau"mateso makubwa waliyopitia na wanayopitia siku baada ya siku.
Suluhisho la serikali mbili
Msimamo wa Vatican, alisisitiza tena, bado siku zote ni sawa kuhitaji: suluhisho la serikali mbili, moja ya Israeli na Palestina. Kwa muda mrefu, na kwa hivyo hata kabla ya mzozo huo wa hivi karibuni na wa kutisha, kufuatia matukio ya ukatili ya mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, Vatican iliunga mkono kanuni hiyo ya ndani ya jumuiya ya kimataifa na ilifanya hivyo hata wakati wengine wengi walikuwa wanaitupilia mbali. Kwa kutazama leo hii ni dhahiri kabisa, kwamba utekelezaji unaowezekana unajadiliwa kwa sababu hali katika maeneo ya Wapalestina ya Ukingo wa Magharibi pia ni mbaya sana, alibainisha Katibu wa Vatican wa Uhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, kuwa “kama kungekuwa na kunyakuliwa kwa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Israeli, ingekuwa vigumu sana kufikiria jinsi gani kunaweza kuwa na matumaini katika siku za usoni za kufikia suluhisho la serikali mbili.” Vatican, alisisitiza wakati huo huo kuwa inaendelea kuunga mkono kwa ujumla wa kusitisha mapigano, kuachiliwa kwa mateka wote, ulinzi wa raia na heshima kamili kwa sheria za kimataifa za kibinadamu. Pamoja na ujenzi wa Gaza, kuimarishwa kwa hali katika maeneo ya Wapalestina ya Ukanda wa Magharibi wa Mto Jordan na heshima kwa watu wa Palestina katika maeneo hayo. Hata hivyo, matarajio yanasalia kuwa ya suluhisho la mzozo kati ya Waisraeli na Wapalestina. Lakini, alisema, kusuluhisha suala la Palestina kunaonekana kama kiini cha matatizo mengi katika Mashariki ya Kati, iwe Syria, Lebanon au maeneo mengine ya kanda.
Mchungaji kwa wote
Alipoulizwa kuakisi umakini wa Papa kwa suala la Israeli na Palestina na simu za mara kwa mara kwa Jumuiya ya Kikatoliki ya Gaza na Paroko wake wa Parokia, ambayo jarida hilo linaripoti "ukosoaji" kutoka kwa "viongozi wa Israeli na Wayahudi,” Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka jinsi ambavyo Papa Francisko daima amejaribu kufikia pande zote mbili za mzozo huu mbaya. "Ni kweli, anajaribu kuwaita Parokia ya Gaza kila jioni, ili kuzungumza na mapadre na kupata habari za watu wanaoishi huko," alisema, akitoa mfano wa "kuthaminiwa sana". Lakini, Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka katika sehemu hii ya mazungumzo na jarida la "Amerika" ambayo pia alijibu maswali mengine, kuhusu afya ya Papa hadi safari zake, kwamba Papa "pia alipokea familia nyingi za mateka," pamoja na kuandika barua kwa “kaka na dada” wa Kiyahudi huko Israeli na barua kwa Wakatoliki katika Mashariki ya Kati: kwa hiyo alijaribu kuwa “mchungaji” kwa wote.