Rais Gitanas Nausèda wa Lithuania Atembelea Mjini Vatican
Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa, Jumatatu tarehe 3 Machi 2025 amekutana na kuzungumza na Rais Gitanas Nausėda wa Lithuania, ambaye anashiriki katika hija ya matumaini ya watu wa Mungu kutoka Lithuania. Rais Nausèda anashiriki katika hija ya matumaini ya watu wa Mungu kutoka nchini Lithuania.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa, Jumatatu tarehe 3 Machi 2025 amekutana na kuzungumza na Rais Gitanas NausÄ—da wa Lithuania, ambaye anashiriki katika hija ya matumaini ya watu wa Mungu kutoka Lithuania.
Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili sanjari na mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Lithuania. Baadaye, viongozi hawa wamejielekeza zaidi katika masuala ya kikanda na kimataifa mintarafu mchakato wa kutafuta na kukuza amani nchini Ukraine.
04 Machi 2025, 15:43