ÐÓMAPµ¼º½

2025.02.18 Alessandra  Smerilli akiwa huko Dakar nchini Senegal 2025.02.18 Alessandra Smerilli akiwa huko Dakar nchini Senegal 

Vatican: Afrika inazidi kuwa tete kutokana na vita na majanga ya asili

Monsinyo Roberto Campisi,Mhusika wa Masuala Mkuu wa Sekretarieti ya Vatican,alizungumza katika mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Yohane Paulo II wa Sahel huko Dakar,Senegal na kuonesha ukaribu wa Papa.Hotuba kutoka katika Baraza la Kipapa la kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Vatican News

Ni fursa ya kushiriki kidugu utume wa kichungaji katika kanda ya Sahel ya Afrika. Haya ndiyo yalikuwa mawazo yaliyotolewa na Monsinyo Roberto Campisi, Mhusika wa Masuala Mkuu wa Sekretarieti ya mji wa Vatican, akizungumza kwenye Kikao cha 43 cha Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mfuko Yohane  Paulo II la Sahel, kilichofunguliwa tarehe 17 Februari na kitahitimishwa tarehe 21 Februari 2025 huko Dakar nchini  Senegal. Monsinyo Campisi katika salamu zake aliwasilisha ukaribu wa Papa kwa Mfuko huo  unaobeba jina la Yohane Paulo II kwa hakika, ni Papa wa Poland aliyetaka kuundwa kwake mnamo mwaka 1984 baada ya ziara yake ya kwanza barani Afrika.

Bara la Afrika ni tete

Mwakilishi wa Sekretarieti ya Nchi  alisema "Bara la Afrika linazidi kuwa tete kutokana na migogoro ya silaha katika baadhi ya nchi za Sahel na kutokana na majanga ya asili." Kwa hiyo, ili kuitikia wito wake ipasavyo, Mfuko wa Yohane  Paulo II unaitwa kuchangia katika maendeleo fungamani ya binadamu lakini pia kueleza mipango yake kulingana na miongozo iliyooneshwa na katiba ya kitume Praedicate evangelium. Akimshukuru Askofu Mkuu wa Dakar, Benjamin Ndiaye, kwa ukarimu uliotolewa kwa Mfuko huo  Mwakilishi wa Vatican alizungumza juu ya "ishara ya usikivu wa kidugu" na "ushuhuda fasaha wa ushirika" kati ya maaskofu ambao shirika la papa limekabidhiwa. Hatimaye, matumaini kwamba mkutano huo pia utakuwa ni fursa ya kutafakari kwa pamoja kanuni mpya zinazosimamia misingi ya Vatican, kufuatia mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wa mageuzi ya Curia Romana  yanayotokana na mageuzi ya ndani kwanza.

Smerilli:Kukabiliana na changamoto za umaskini, ukosefu wa haki kwa kuishi pamoja kwa amani

Katika hotuba yake nchini Senegal, Sr Alessandra Smerilli, katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma Fungamani ya Binadamu, alisisitiza haja ya kushughulikia ukosefu wa haki ambao ni chanzo cha migogoro katika Kanda ya Sahel pia. Mwaliko huo ni kuungana na nguvu na Papa katika mapambano dhidi ya umaskini, katika kufikia maendeleo fungamani ya binadamu kwa kaka na dada zetu wote na katika kutafuta kuishi pamoja kwa amani kati ya watu wa Sahel. Hii ndiyo changamoto kubwa inayotungoja leo." Mtawa huyo aliwashukuru kwa kujitolea kwao katika vita "kwa ajili ya Afrika iwe bora, ambapo hakuna hadhi ya  mtu inayokanyagwa na ambapo udugu unakuwa ukweli, chanzo cha furaha na matumaini kwa wote." Akikumbuka mitazamo mipya iliyooneshwa na mageuzi ya mifuko ya kipapa, Sista Smerilli anatumaini kwamba hatua zinazotekelezwa zinaweza kuakisi "tunu za ulimwengu za haki, mshikamano na huruma, na zinaelekezwa kwenye manufaa ya wote na kuelekea kufanya kazi kwa ajili ya amani na urafiki wa kijamii, na kuleta mabadiliko kwa ajili ya maendeleo fungamani ya ubinadamu katika Kanda ya Sahel."

Utume wa Sahel
19 Februari 2025, 11:10